• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 2:25 PM
Wasichana wengi zaidi wakeketwa msimu wa Krismasi

Wasichana wengi zaidi wakeketwa msimu wa Krismasi

NA OSCAR KAKAI

Visa vya ukeketaji vimeongezeka katika msimo huu wa Krismasi katika Kaunti ya Pokot Magharibi. Kulingana na wanaharakati wanaopigana na visa hivyo katika kaunti hiyo, visa vingi vya tohara ya wasichana vimeripotiwa likizo hii ya mwezi wa Desemba.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Kapenguria Theatres Bw Francis Soprin alisema kuwa visa hivyo vimeongezeka kutoka asilimia 75 hadi 78 sababu ya kipindi kirefu cha likizo.

Bw Soprin alisema kuwa wasichana wengi wamejeruhiwa sehemu nyeti baada ya kukeketwa msimu huu . “Visa hivi vimeongezeka sababu ya wakazi kukosa habari, kiwango cha juu cha kukosa mafunzo na kupuuza mambo,” alisema.

Akiongea mjini Kapenguria kwenye hafla ya kuwapa mafunzo wasichana kuhusiana na ukeketaji na kupata njia mbadala, Bw Soprin alisema kuwa wavulana wengi walitairiwa katika eneo hilo suala ambalo lilichangia wasichana kutaka kukeketwa ili kuwa kama wao.

“Wengi hawana habari kuhusu athari za ukeketaji .Wengi huvuja damu baada ya kukatwa,”alisema Bw Soprin.

Bw Soprin alisema kuwa kikundi hicho kimeweka mikakati kumaliza visa hivyo kwa kufika katika vijiji vya mashinani penye visa hivyo hutelelezwa kwa wingi.

“Tumejaribu kufika maeneo ambayo yanakumbwa na shida hiyo na wala sio kufanyia mikutano mikahawa mikubwa ya Kitale Nairobi.Tunawarai washikadau ili kushirikiana kupigana na visa hivi kwa kufikia wale ambao wameathirika .Tunahitaji mchango wa kila mtu,”alisema.

Alisema kuwa serikali ya kaunti na ya kitaifa yaijatambua shida kama suala kuu.

“Wangechukua muda kufikiria kuhusu sehemu ambayo hukatwa,”alisema. Wasichana hao walitolewa katika vijiji vya Sina ,Sopukwo,Sendros ,Kachemgon, Samich na kupata mafunzo ya siku nne kwenye warsha iliyoandaliwa katika shule ya msingi ya Samich.

Bw Soprin alisema kuwa mafunzo hayo yaliwawezesha kuelewa athari za kukeketwa .

“Huu ni mfano wa kubadilisha sherehe ambazo hufanywa na tunataka jamii kuwatambua wasichana,”alisema.

Mratibu wa shirika hilo Bw Sammy Abuyanza alisema kuwa wanasiana wamechangia kwa ongezeko la visa hivyo sababu hawajajitokeza kuzungumizia suala hilo.

“Kwa miaka saba tumekuwa tukitumia machifu ,wazee wa mitaa ,vikundi vya kijamii na walimu na tumeona magtunda.Tunataka viongozi kujitokeza,” alisema.

Alisema kuwa visa hivyo vimeongezeka katika maeneo ambapo wakazi hawajakumbatia elimu .

“Kuna shida katika maeneo ya Masol,Takaywa na Nyangaita ambapo visa hivyo vimeongezeka. Katika maeneo mengine kama Nyarkulian, Sondany na Koporo wasichana kukeketwa kisiri .Tunataka walimu kusaidia kumalza visa hivi,” Bw Abuyanza alisema.

You can share this post!

SHAIRI: Msirarue maisha yangu

Jinsi ya kukwepa wahalifu unapomumunya Krismasi