• Nairobi
  • Last Updated September 26th, 2023 10:25 PM
Wavuvi wauana kwa sababu ya sigara ya Sh15

Wavuvi wauana kwa sababu ya sigara ya Sh15

NA GEORGE ODIWUOR

WAVUVI wawili kutoka kisiwa cha Rusinga, Kaunti ya Homa Bay, walipoteza maisha kufuatia ugomvi kuhusu sigara ya Sh15.

Sikuku Odiko, mwenye umri wa miaka 36, alimuua kwa kumdunga kisu rafikiye wa muda mrefu Geoffrey Ngoje, 32, kabla ya umma kumshambulia na kumuua.

Kisa hicho kilitendeka kwenye ufuo wa Nyagina eneo la Rusinga Mashariki mnamo Jumamosi jioni, Septemba 16, 2023.

Yote yalianza wakati Ngoje aliposhikwa na hamu ya sigara na kununua msokoto wa Sh15 katika duka moja kwenye ufuo wa Nyagina.

Alipokuwa akivuta, mvuvi mwenzake, Odiko, aliyemwona akienda dukani lakini hakuwa na hela za kununua wakati huo vilevile alishikwa na hamu.

“Alimshambulia mwenzake kwa kumnyima sigara. Walianza kugombana kuhusu suala hilo kabla ya vifo kutokea,” alisema Chifu wa Rusinga Mashariki, Mboya Owuor.

 

  • Tags

You can share this post!

Utalii Lamu unavyoyumbishwa na mfumko wa bei ya mafuta ya...

Khalwale ahimiza Ruto kufuta mawaziri wanaompotosha

T L