• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
Wetang’ula awatetea majaji 5 kuhusu BBI

Wetang’ula awatetea majaji 5 kuhusu BBI

Na BRIAN OJAMAA

KINARA wa chama Ford Kenya, Bw Moses Wetang’ula amewataka wanasiasa na Wakenya wakome kuwatusi majaji watano waliotoa uamuzi wiki jana kuwa Mpango wa Maridhiano (BBI) ni haramu na haufuati katiba.

Seneta huyo wa Bungoma, badala yake, alimtaka Rais Uhuru Kenyatta kuandaa kikao na viongozi waliokuwa wakipigia upato BBI ili kuyashughulikia masuala yaliyoibuliwa na majaji hao watano.

Akizungumza wakati wa hafla ya mazishi katika eneobunge la Kabuchai, Bw Wetang’ula alimtaka Rais kuwaleta viongozi wote wa kisiasa ili kuona namna utata unaokabili BBI utakavyotatuliwa.

“Majaji hao watano kama tu watu wengine, wanaweza kufanya makosa na uamuzi wao pia unaweza kuwa una dosari,” akasema Bw Wetang’ula.

Alikiri kwamba uamuzi huo ulikuwa umetia breki mchakato wa BBI ilhali kila mtu alikuwa ashaelekeza macho katika kura ya maamuzi.

Vilevile Seneta huyo wa Bungoma alitaka sekretarieti ya BBI itafute huduma za mawakili wazoefu wenye tajriba kuwasilisha rufaa hiyo na kukosoa uamuzi wa majaji watano, huku akieleza imani yake kuwa rufaa hiyo itapita.

You can share this post!

Jumwa ajipiga kifua baada ya ‘Reggae’ kuzimwa

Uhuru apangiwa kuzuru Pwani baada ya Raila