• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Wezi wavamia hospitali na kupora wagonjwa

Wezi wavamia hospitali na kupora wagonjwa

Na WANGU KANURI

WEZI waliojihami kwa bunduki walivamia hospitali moja ya kibinafsi katika eneo la Ruai, kaunti ya Nairobi na kupora wagonjwa.

Wahalifu hao wanadaiwa kutoroka na simu pamoja na pesa.

Kwa mujibu wa walinda lango katika hospitali ya Ruai Family, wezi hao waliokuwa wakiendesha pikipiki, walivamia kituo hicho cha afya mnamo Jumatatu, Aprili 10 saa kumi asubuhi.

Walipofika hospitalini, walifyatua risasi moja hewani iliyosababisha wafanyikazi pamoja na wagonjwa kulala chali sakafuni.

Mmoja wa wezi hao aliokota simu nne kutoka kwa wagonjwa waliokuwa hospitalini na pesa ambazo kiwango chake hadi kufikia sasa hakijajulikana.

Baadaye walihepa kwa kutumia pikipiki iliyokuwa ikiwangoja.

Hata ingawa hakuna mtu aliyejeruhiwa, polisi walisema bado kuwa hawajamshika mtu yeyote anayehusishwa na uvamizi huo hospitalini.

Vile vile, wanasema kuwa wezi hao walikuwa kwenye shughuli za kuwapora watu mali yao walipoamua kuingia katika hospitali hiyo ya kibinafsi.

Timu ya makachero ilifika katika hospitali hiyo Jutatu na Jumanne, na kupekua kamera za CCTV zinazoonyesha jinsi wezi hao walitekeleza uwizi huo.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Nairobi Adamson Bungei alisema kuwa wanashirikiana na polisi katika kaunti ya Kiambu ili kuwakamata wezi hao.

Kisa hicho cha kushangaza kinajiri siku chache baada ya majangili eneo la Iten, kuvamia hospitali na kuokoa mmoja wao aliyekuwa akiendelea kupata matibabu.

Kitendawili cha uvamizi huo kufikia sasa kimesalia kukosa mteguzi, duru zikihoji angili huyo alikuwa chini ya ulinzi wa askari.

 

  • Tags

You can share this post!

Wanasiasa wa Azimio wapinga uteuzi wa Keynan

CECIL ODONGO: Mbona KKA wana kiwewe sava ya IEBC...

T L