• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:09 PM
Wizi wa mafuta ya transfoma unavyoacha wakazi wa Maai-Mahiu, Suswa kwenye giza kila mara

Wizi wa mafuta ya transfoma unavyoacha wakazi wa Maai-Mahiu, Suswa kwenye giza kila mara

NA RICHARD MAOSI

Wezi katika kituo cha kibiashara cha Maai Mahiu – Suswa kwa siri wanauza mafuta ya transfoma kwa wachuuzi wa chakula kandokando ya barabara.

Ikiaminika mafuta haya yanatumika kuandaa mapochopocho kama vile maandazi na chipsi.

Lakini athari zake zimewafanya wenyeji kuzoea maisha  ya giza, kutokana na stima kupotea mara kwa mara hasa pale transfoma zinapoangushwa na kuibiwa.

Miaka ya awali ilianza kama mchezo kwa kuiba mafuta ya transfoma, ambayo hatimaye huchuuzwa mitaani kwa wauzaji wa vibanzi kwa bei ya rejareja.

“Lakini wakaerevuka biashara ya vyuma kuukuu nchini ilipoanza, sasa ikawa sio wizi wa mafuta tu bali pia nyaya za copper na transfoma,” asema Bi Esther Mwakiru

Mwakiru ni dobi na hutumia umeme wa stima kusafisha na kukausha nguo ila amekuwa akikadiria hasara kutokana na idadi ndogo ya wateja ambao hutembea kioski chake kidogo.

Anasema Maai Mahiu ni mojawapo ya maeneo nchini, ambayo hutoa mazingira mazuri kwa madereva wa shughuli za uchukuzi wa masafa marefu kupumzika.

Isitoshe biashara za mikahawa, kumbi za burudani ni baadhi ya vivutio vya kipekee kwa wageni kutoka Kaunti jirani za Nakuru, Nairobi, Kiambu na Narok.

Mnamo 2021 polisi walinasa zaidi ya lita 3,000 ya mafuta ya transfoma ambayo yalikuwa yakielekea katika sehemu isiyojulikana.

Mfanyabishara Erick Omondi ambaye anamiliki mkahawa katika barabara kuu ya Maai Mahiu ukielekea kituo cha kibiashara cha Suswa anasema swala la kupotea kwa umeme katika eneo hili ni jambo la kawaida.

Anasema mnamo Mei Mwaka huu wakazi wenye hasira kutoka mtaani Kihoto walifunga barabara kwa kulalamikia Shirika la Usimamizi wa Umeme KPLC kwa kukosa kubadilisha transfoma.

Alifichulia Taifa Leo Dijitali kwamba kituo cha Reli ya Kisasa eneo la Suswa kinamiliki transfoma ambayo inaweza kuwasha vijiji vinne.

Lakini mara nyingi wamekuwa wakishinda gizani kutokana na visa vya wezi kuharibu au kuiba mafuta kutoka kwenye transfoma.

Anasema huenda wezi wamekuwa wakishirikiana na polisi au wafanyikazi wa Shirika la KPLC kuwahangaisha kwani wakati mwingine huchukua muda mrefu kabla ya malalamishi yao kuangaziwa.

Isitoshe wezi wamekuwa wakiwauzia wamiliki wa baadhi ya mikahawa hapa mafuta haya ambayo huuzwa kwa bei nafuu na hutumika kuandaavibanzi na vyakula.

  • Tags

You can share this post!

Wakenya wakisota, kuna Sh28 milioni zimekosa wenyewe...

Viatu vya Uhuru sasa vyamfinya Rais William Ruto

T L