• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:05 PM
Wakenya wakisota, kuna Sh28 milioni zimekosa wenyewe Nyandarua

Wakenya wakisota, kuna Sh28 milioni zimekosa wenyewe Nyandarua

KNA na LABAAN SHABAAN

Yamkini kuna wananchi wanalala njaa sasa kwa sababu mifuko yao imetoboka lakini hawajui pesa zao ziko kortini zinawasubiri.

Wakenya wanapolia kuwa wamesota na hali ya maisha kuwa ngumu, mahakama ya Nyahururu imewaomba walioweka dhamana ya pesa taslimu kortini ya kima cha zaidi ya Sh20 milioni waendee fedha zao.

Sehemu ya pesa hizo zimekuwa kortini kwa takriban miongo mitatu na sasa mahakama imeonya kuwa endapo wenye fedha hizo hawatajitokeza, zitakabidhiwa kwa Mamlaka ya Mali Zisizodaiwa (UAA).

Kwa mujibu wa sheria, UAA inafaa kutwaa fedha hizo ndani ya miaka mitatu iwapo wenyewe hawatazidai.

Hakimu Mkuu Jaji Evans Keago ambaye ni mkuu wa mahakama ya Nyahururu amedokeza uwezekano wa wakenya kutojua mchakato wa kudai dhamana zao.

“Tuna faili lakini hatuna nambari za mawasiliano ya wenye pesa hizo na tunarai manaibu kamishna wa kaunti watusaidie kuhamasisha umma kuhusu dhamana zisizokusanywa,” alisema Bw Keago akiwaambia wanaodai pesa hizo watahitajika kutoa ithibati na kujitambulisha kwa usahihi.

Kuna dhamana 2,114 ambazo hazijachukuliwa huko kortini na kati ya hizo, dhamana ya pesa taslimu 297 zimeganda mahakamani kwa zaidi ya miaka 20.

Pesa hizo ni kati ya Sh1000 na Sh100, 000 jumla zikifika Sh 28,072,854.70 kulingana na rekodi ya Aprili 2023.

  • Tags

You can share this post!

NILIKUSALITI, NISAMEHE: Mbunge wa zamani wa Kesses Swarup...

Wizi wa mafuta ya transfoma unavyoacha wakazi wa...

T L