• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Zuma airai korti itathmini hukumu iliyotoa dhidi yake

Zuma airai korti itathmini hukumu iliyotoa dhidi yake

ALIYEKUWA rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, anaitaka Mahakama ya Kikatiba nchini humo kutathmini upya hukumu iliyotoa dhidi yake kwa kukwepa kuhudhuria vikao vya mahakama.

Kiongozi huyo alihukumiwa miezi 15 gerezani Jumanne wiki iliyopita kwa kukosa kuhudhuria msururu wa vikao vya mahakama kutokana na kesi ya ufisadi inayomkabili.Zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya muda ambao kiongozi huyo alipewa na mahakama kujisalimisha kwa polisi kuisha, Zuma amewasilisha rasmi ombi lake mahakamani akiomba hukumu hiyo kuangaliwa upya.

“Ninaiomba mahakama kutenga muda na kutathmini tena hukumu iliyotoa dhidi yangu. Ingawa ilizingatia taratibu za kisheria katika utoaji adhabu hiyo, haifai kulingana na umri na hali yangu kiafya,” akasema Zuma kwenye stakabadhi alizowasilisha mahakamani Ijumaa.

Baadhi ya mawakili wamesema kuwa bado kuna uwezekano kwa mahakama kutathmini upya ombi hilo, ili kubaini ikiwa ilizingatia Katiba ama ilikiuka mamlaka yake katika utoaji wa kifungo hicho.Vile vile, ameirai Mahakama Kuu kuchelewesha utekelezaji wa hukumu hiyo ili kutoa nafasi kwa ombi lake kutathminiwa.

Kwenye uamuzi wake, mahakama haikumpata tu na hatia ya kukwepa kuhudhuria vikao vyake, bali pia na kosa la kuihadaa na kuupotosha umma.Hata hivyo, washauri wake wamesema daima atakuwa akizingatia sheriaBaada ya hukumu hiyo, Zuma alipewa siku tano kujisalimisha kwa polisi, la sivyo akamatwe.

Alipohudumu kama rais, Zuma aliandamwa na madai ya msururu wa sakata za ufisadi.Wafanyabiashara maarufu walilaumiwa kwa kupanga njama na wanasiasa wenye ushawishi kupata kandarasi serikalini. Zuma aling’atuka uongozini 2018.Kiongozi huyo wa zamani alifika mahakamani mara moja tu lakini akakataa kufika katika vikao vingine vilivyofuata.

Kiongozi wa jopo maalum lililobuniwa kumchunguza—Jaji Sisi Khampepe—aliiomba Mahakama ya Kikatiba kuingilia kati.Akitoa uamuzi wake, Kaimu Jaji Mkuu Sisi Khampepe alisema “hatua ya Zuma kutofika mahakamani ilidhihirisha ukosefu wa hekima kwa Idara ya Mahakama.”“Sikuachwa na uamuzi mwingine ila kumfunga gerezani Zuma.

Lengo langu ni kutoa onyo na ujumbe mkali. Ni lazima taratibu za kisheria ziheshimiwe,” akaeleza kwenye uamuzi wake.Zuma hakuwa mahakamani wakati wa utoaji wa adhabu hiyo. Kiongozi huyo amekuwa akisisitiza kwamba kesi hiyo inatokana na njama za kisiasa zinazoendeshwa na wapinzani wake.

Mwezi uliopita, Zuma alikana tuhuma kuwa alijifaidi kwenye sakata ya ununuzi wa silaha ya Sh500 bilioni katika miaka ya tisini.Wakosoaji wa hukumu hiyo wanaitaja kuwa njama ya serikali ya Rais Cyril Ramaphosa kumwadhibu Zuma na washirika wake.Uamuzi huo pia umetajwa kuwa na athari za kisiasa kwa chama tawala, ANC.

  • Tags

You can share this post!

Covid: Utafiti mpya wahimiza manufaa ya kupokea chanjo

OCS kufikishwa kortini leo kwa madai ya kuchukua hongo