• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
OCS kufikishwa kortini leo kwa madai ya kuchukua hongo

OCS kufikishwa kortini leo kwa madai ya kuchukua hongo

ERIC MATARA na JOHN NJOROGE

KAMANDA wa Kituo cha Polisi cha Molo Anne Kanori anatarajiwa kufikishwa kortini leo kwa madai ya kuchukua hongo.

Kamanda huyo wa polisi alikamatwa Ijumaa na kuzuiliwa katika seli ya Kituo cha Polisi cha Railways mjini Nakuru.Maafisa wanne wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) Ijumaa walimnasa Kanori baada ya kuvamia kituo hicho cha polisi.

Kulingana na EACC, maafisa wake walimkamata Kanori baada ya kupokea malalamishi kutoka kwa wakazi wa Nakuru kuwa kamanda huyo wa polisi alikuwa akijihusisha na visa vya ufisadi.Maafisa wa EACC walimpata Kanori na Sh10,000 zilizotumika kumtega baada ya kutiwa alama.

Kamanda huyo wa polisi atafikishwa kortini na maafisa wengine wanne kutoka Kituo cha Polisi cha Molo ambao wanadaiwa kushambulia maafisa wa EACC.Wanne hao ni Emilly Atsieno, Peter Lemuli, Eveline Chepkoech naErick Kibet ambao wanazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Nakuru Central.

Kabla ya kumkamata afisa huyo, kulikuwa na kizaazaa huku maafisa wa EACC wakijaribu kumpokonya bunduki.Bi Kanori alipiga mayowe na kusababisha wenzake kufika kwa haraka ili kumsaidia.

Polisi hao waliwakamata maafisa wa EACC na kuwazuilia kituoni bila kuandika katika kitabu cha rekodi za matukio ya kila siku.Ripoti ya polisi inaonyesha kuwa maafisa wa EACC; Abdi Muktar, Nancy Kirui na Mildred Miloya walijeruhiwa na polisi.

  • Tags

You can share this post!

Zuma airai korti itathmini hukumu iliyotoa dhidi yake

Wadau wa Pwani wataka Ligi Kuu ya Drafu ianze nchini