• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Daraja la kuunganisha Murera na Kalimoni lazinduliwa

Daraja la kuunganisha Murera na Kalimoni lazinduliwa

Na LAWRENCE ONGARO

WAKAZI wa Murera na Kalimoni watanufaika pakubwa baada ya daraja la kuunganisha maeneo hayo kukamilika.

Mnamo Jumatatu, Gavana wa Kiambu Dkt James Nyoro, alifungua daraja hilo kwenye hafla ambapo wakazi wa maeneo hayo walipongeza juhudi hizo.

Kwa muda mrefu, wakazi wa maeneo hayo wamepitia changamoto tele na wakilazimika kuzunguka mwendo mrefu.

Dkt Nyoro alisema ni afueni sasa kwa wakazi wa Murera, Kalimoni na Juja kupata daraja jipya.

“Kwa hakika daraja hilo litanufaisha waendao kwa miguu, wahudumu wa bodaboda  na pia wafanyabiashara. Kila mkazi wa eneo hilo atanufaika pakubwa huku maendeleo yakipatikana,” alisema Dkt Nyoro.

Hapo awali wakazi wa eneo hilo walipitia changamoto tele kwa sababu kuliponyesha mvua, shughuli za masomo zilikwama kwa muda kwa sababu ya ubovu wa barabara hiyo. Ndivyo alifafanua gavana huyo.

Ilidaiwa wanafunzi wengi walilazimika kuzunguka kilomita zaidi ya tano hivi ili kufika shuleni.

Wakati wa kuzinduliwa kwa daraja hilo, wakazi wengi walielezea masaibu yao huku wakipongeza juhudi za kaunti ya Kiambu kutengeneza daraja hilo.

Wakati wa ziara hiyo gavana Nyoro, aliandamana na maafisa wakuu wa kaunti ambao walipongeza juhudi za kaunti hiyo kuleta maendeleo.

Bw Joseph Kamau aliye mkazi wa kijiji cha Murera alisema sasa wataendesha biashara zao bila kutatizika.

“Tunashukuru serikali ya kaunti ya Kiambu kupitia gavana wetu Nyoro, kwa kutujengea daraja jipya ambalo halikuwepo hapo awali. Sasa tutapata maendeleo makubwa,” alisema  Bw Kamau.

Bw Peter Maina kutoka Kalimoni anasema wanafunzi watapata afueni baada ya kutaabika kwa muda mrefu wakipitia mwendo mrefu,” alifafanua Bw Maina.

Bi Jane Muthoni wa kutoka Juja alisema watapata nafasi kuzuru maeneo ya Murera na Kalimoni ili kununua vyakula kwa urahisi.

“Tumepata taabu hasa wakati mvua inaponyesha. Huwa kuna mafuriko ya maji na inatubidi sisi wakazi wa eneo hili kuzunguka mwendo mrefu,” alifafanua Bi Muthoni.

Kulingana na wakazi hao, daraja hilo ni thabiti na limeundwa kwa muundo wa kisasa.

You can share this post!

Eric Omondi ashauriwa ajihusishe kikamilifu na majukumu ya...

‘Fimbo ya Malkia Elizabeth inaunganisha mataifa ya...

T L