• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Jinsi madiwani walivyokunja mkia wakaachana na mpango wa kumtimua Orengo

Jinsi madiwani walivyokunja mkia wakaachana na mpango wa kumtimua Orengo

NA KASSIM ADINASI

SASA imefichuka kwamba madiwani waliopanga kumtimua Gavana wa Kaunti ya Siaya James Orengo wamekunja mkia baada ya kiongozi huyo kukaa ngumu na kukataa wao kuwa na ushawishi kuhusu miradi kadhaa katika wadi zao.

Madiwani hao, kulingana na chanzo ndani ya serikali ya kaunti, walitaka kumtisha Gavana Orengo kwa hoja ya kumtimua ili aingize baridi na akubali kuwarudishia mkono.

Afisa aliyezungumza na Taifa Jumapili kwa ahadi kwamba asitajwe, amesema sasa hakuna hata diwani mmoja anayetaka kuhusishwa na njama hiyo ya kumtimua Gavana Orengo ambaye ni wakili mwenye tajriba ya juu.

“Hoja zilizolenga kumtimua Gavana Orengo na Waziri wa Fedha wa Kaunti ya Siaya Benedict Omolo zilikuwa zimetayarushwa ikiwa matakwa na masharti yao yangepuuzwa,” chanzo hicho kimesema.

Lakini kulingana na chanzo, “Gavana alikataa katakata kukubali matakwa ya madiwani hao. Aliwaambia wazi kwamba hawezi akawapa tenda au kampuni zinazohusishwa na madiwani hao kwa sababu kufanya hivyo kungekuwa ni kuenda kinyume na sheria.”

Bunge la Kaunti liligawanyika kwa makundi mawili, moja likishabikia kutimuliwa kwa gavana huku la pili likipinga.

Kwenye mazishi ya Mama Mary Msando mnamo Oktoba 28, 2023, katika eneo la Lifunga Kobiero katika kaunti ndogo ya Ugenya, baadhu ya madiwani walizomewa na waombolezaji kwa kuonyesha tamaa ya kunyemelea pesa za maendeleo ya wadi kadhaa katika Kaunti ya Siaya.

[email protected]

  • Tags

You can share this post!

Videge wapendanao wageuza hoteli jukwaa la kulumbana

Wakenya sasa wageukia unga wa ‘kisiagi’ kupunguza...

T L