• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:55 AM
Kibicho alalama kuhusu idadi ndogo ya watu waliojisajili

Kibicho alalama kuhusu idadi ndogo ya watu waliojisajili

Na GEORGE MUNENE

KATIBU wa Usalama wa Ndani, Bw Karanja Kibicho, amelalamikia idadi ya chini ya vijana ambao wamejitokeza kujisajili kama wapigakura katika Kaunti ya Kirinyaga.

Bw Kibicho alisema kuwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), ilikuwa ikilenga kuwasajili wapigakura wapya 130,000 ila ni 20,000 pekee ambao wamejisajili kufikia wikendi.

“Ni aibu kuwaona vijana na wakazi ambao hawajajisajili kama wapigakura wakirandaranda tu,” akasema mnamo Jumamosi katika eneo la Karira, eneobunge la Mwea.

Alionya kuwa wengi huenda wakafungiwa nje ya kura ya 2022 kwa kuwa hawatakuwa na uwezo wa kuwachagua viongozi wapya kama idadi hiyo haitapanda kufikia makataa ya kujisajili yaliyowekwa na IEBC.

“Kama watu wetu hawataki kujisajili kama wapigakura basi watu ambao hawastahili kushikilia vyeo vya uongozi ndio watachaguliwa. Serikali italazimika kuingilia kati na kuwashawishi raia wajisajili,” akaongeza.

You can share this post!

Wahitimu 1,725 wa Thika Technical washauriwa watumie ujuzi...

UDAKU: Binti wa Guardiola abaki kwa mataa Dele Alli...

T L