• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Mama kortini kukiri kuua mwanawe

Mama kortini kukiri kuua mwanawe

Na TITUS OMINDE

Mwanamke mwenye umri wa miaka 27 aliishangaza mahakama kuu ya Eldoret alipokiri kumuua kinyama na kumzika mtoto wake mgonjwa.

Mwanamke huyo alidai kuwa aliua mtoto huyo kwa kukosa pesa za kumpeleka kwa matibabu katika hospitali moja ya eneo hilo.Mshitakiwa huyo, Rose Angelina, aliiambia mahakama kuwa alimfanyia mtoto huyo kitendo hicho baada ya baba yake kukosa kuajibikia majukumu yake kama mzazi na kumuachia mzigo wote wa ulezi tangu alipozaliwa mwaka mmoja uliopita.

Bi Angelina alisema kuwa mtoto huyo amekuwa akiugua ugonjwa wa muda mrefu, hata hivyo hakuambia korti aina ya ugonjwa husika.’Ningependa kukiri kwa mahakama hii kwamba nilimuua mtoto wangu aliyekuwa mgonjwa kama ilivyoonyeshwa kwenye maelezo ya mashtaka, kisha baadaye nilimzika kwenye kaburi lisilo na kina kirefu,’ aliambia mahakama Angelina alipofika mbele ya jaji Eric Ogola.

Mshtakiwa, ambaye hufanya kazi ya vibarua, alitenda kosa hilo mnamo tarehe 12 Januari 2017 katika kijiji cha Chikuli Kaunti Ndogo ya Lugari Kaunti ya Kakamega.Angelina alimsihi jaji amwachilie kwa bondi akisema amekaa katika gereza la Eldoret tangu alipokamatwa na maafisa wa polisi kutoka idara ya upelelezi wa makosa ya jinai mwaka wa 2017.

Alimwambia Jaji kwamba hakuna hata mmoja wa wanafamilia wake wa karibu aliyewahi kuja kumtembelea katika kituo cha kurekebisha tabia tangu akamatwe siku ya maafa aliyoshtakiwa kumuua mtoto wake.“Heshima yako hakuna jamaa yangu miongoni mwao mama yangu ambaye amewahi kuja kunitembelea katika gereza la Eldoret GK.

Ninaomba uniachilie kwa dhamana kwa sababu ninateseka gerezani,” alimwambia Hakimu.Alipoulizwa na Hakimu atakwenda wapi iwapo ataachiliwa kwa bondi sasa ambapo inaonekana hakuna ndugu yake anayetaka kushirikiana naye baada ya kuhusishwa na mauaji ya kikatili ya mtoto wake, alijibu kuwa angesafiri hadi mjini Kitale na kukaa huku mjomba wake akisema kuwa anaelewana naye.

Hakimu Ogola alisema kuwa atatoa uamuzi kuhusu ombi lake la kuachiliwa kwa dhamana mnamo Mei 11, 2022 na kuagiza mshtakiwa asindikizwe hadi katika gereza la wanawake la Eldoret GK.

You can share this post!

Museveni atetea kutuma jeshi DRC

Kundi la wanakijiji tajiri lenye ushawishi mkubwa

T L