• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 9:50 AM
Kundi la wanakijiji tajiri lenye ushawishi mkubwa

Kundi la wanakijiji tajiri lenye ushawishi mkubwa

Na WANDERI KAMAU

WAKFU wa Mlima Kenya (MKF) umeibuka kuwa wenye ushawishi mkubwa, hasa kwenye siasa zinazoendelea za kumrithi Rais Uhuru Kenyatta mwaka ujao.

Je, chimbuko lake ni lipi?Wakfu huo ulianzishwa mwanzoni mwa miaka ya tisini na mabwanyenye kadhaa wa Kaunti ya Murang’a, lengo lao likiwa kuwaunganisha wanataaluma wa kaunti hiyo kushughulikia masuala ya kisiasa na kiuchumi.

Kulingana na waanzilishi wake, lengo lao la kubuni wakfu huo lilitokana na ‘ukatili’ wa serikali ya marehemu Daniel Moi kulitenga eneo lA Mlima Kenya kwenye utawala wake wa miaka 24 kati ya 1978 na 2002.Waanzilishi wakuu wa wakfu huo ni aliyekuwa mwenyekiti wa Benki ya Equity, Peter Munga, Afisa Mkuu Mtendaji wa Benki hiyo, Dkt James Mwangi, bwanyenye SK Macharia kati ya watu wengine matajiri.

“Tulihisi eneo la Mlima Kenya lilihitaji kuwa na sauti ya kulitetea kiuchumi na kisiasa,” akasema Bw Munga.Ingawa liliasisiwa na mabwanyenye wachache tu kutoka Murang’a, limeweza kuvutia uanachama wa watu maarufu kutoka karibu kila pembe ya Mlima Kenya.

Wanahistoria na wadadisi wa siasa za ukanda huo wanasema uwepo wa wanasiasa kama wanachama wak, japo kichinichini, ndiyo sababu kuu ambayo imeujenga na kuinua hadhi yake kuwa wenye ushawishi sana.“Ukitathmini kwa kina, ni vigumu kubaini ikiwa watu kama Mzee Kibaki au Rais Kenyatta wamekuwa wakihusika pakubwa na kufadhili shughuli mbalimbali za wakfu huo.

Hiyo ndiyo sababu imeufanya kutwaa usemi wa mwelekeo wa siasa za eneo hilo kwa kupata ‘baraka’ za Rais Kenyatta,” asema Prof Macharia Munene, ambaye ni msomi wa historia na mchanganuzi wa siasa.

You can share this post!

Mama kortini kukiri kuua mwanawe

IEBC yaonya Raila, Ruto kuhusu kampeni

T L