• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 5:17 PM
Naibu Rais asifia juhudi za Ruto kujitolea kuwekeza katika elimu

Naibu Rais asifia juhudi za Ruto kujitolea kuwekeza katika elimu

NA WACHIRA MWANGI

NAIBU Rais Rigathi Gachagua ameunga mkono juhudi za kujitolea kwa Rais William Ruto kuwekeza katika elimu bora.

Bw ambaye alizungumza katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya mtakatifu Thomas, Kaunti ya Kilifi alibainisha kuwa elimu bora ni muhimu katika kuendesha teknolojia na ubunifu kwa ajili ya maendeleo.

Wakati akiwasilisha basi la shule lenye uwezo wa kubeba abiria 67 kwa shule hiyo, Rigathi alisisitiza haja ya mtoto wa kike kufanya kazi kwa bidii ili nchi ipate manufaa ya kuwekeza katika elimu yao.

“Tuna furaha kuwa hapa asubuhi ya leo. Inatia moyo kuona wasichana wenye nguvu, makini na wenye nia thabiti, ambao wanafanya Mitihani ya Kenya ya Sekondari na ambao wameahidi kufanya vyema wawezavyo. Hii ndiyo njia ya kufuata, nataka mkae makini, mfanye kazi kwa bidii na mjue kuna mahali pa wasichana na wanawake katika kujenga Kenya,” Bw Rigathi alisema.

Huku akiwatia moyo wasichana, Naibu Rais aliongeza kuwa katika Baraza la Mawaziri, kuna Makatibu 8 wa Baraza la Mawaziri ambao wanafanya kazi nzuri sana.

Bw Rigathi alikuwa ameandamana na Gavana Gideon Mung’aro (Kaunti ya Kilifi), Owen Baya (Mbunge wa Kilifi Kaskazini), Waziri wa Madini Salim Mvurya (Uchumi wa Madini), Mwakilishi wa akina Mama Kaunti ya Taita Taveta Lydia Haika na wengineo.

 

  • Tags

You can share this post!

Jamii yaambiwa ndoa za wake wengi huwaweka wanawake kwa...

Ukitumia fomula za wanaojifanya wajuaji utaua penzi lako...

T L