• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:50 AM
Thika mbioni kupata hadhi ya ‘smart city’

Thika mbioni kupata hadhi ya ‘smart city’

NA LAWRENCE ONGARO

MJI wa Thika unatarajiwa hivi karibuni kuwa ‘smart city’ hivi karibuni, Gavana wa Kiambu Bw Kimani Wamatangi akisema mikakati ya kufanikisha mpango huo inaendelea.

“Mpango huo ukifanikiwa wakazi wengi wa Thika na vitongoji vyake hasa wafanyabiashara watanufaika pakubwa,” alisema Bw Wamatangi mnamo Jumanne mjini Thika alipopeana fedha za basari kwa wanafunzi wapatao 2,000.

Mpango huo utagharimu Sh1.5 bilioni.

Bw Wamatangi alisema kwa wakati huu serikali kuu imesambaza Sh400 milioni za kutumika  kujenga soko kuu la Madaraka lililoko eneo la Makongeni mjini Thika.

Mradi huo ukikamilika, wachuuzi wapatao 6,000 watanufaika pakubwa.

Gavana ameahidi kuongeza Sh300 milioni zaidi zitakazosaidia kujenga soko la kisasa eneo la Ngoliba na katika eneo la Jamhuri mjini Thika.

“Masoko hayo yatakapokamilika, tutahakikisha kila mchuuzi wa vyakula anapata mahali pa kuuzia bidhaa zake,” alisema gavana huyo.

Vile vile Bw Wamatangi amewahimiza viongozi waliochaguliwa na wananchi watekeleze wajibu wao ipasavyo bila kujihusisha na siasa za malumbano na vijembe kila mara.

Kuhusu basari, alisema hakuna mwanafunzi anayestahili kubaki nyumbani wakati huu ambapo shule zinafunguliwa.

Alisema mwezi ujao wa Septemba ataongeza fedha kiasi cha Sh100 milioni ili kuwanufaisha wanafunzi wanaorejea shuleni.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na madiwani, washika dau wa elimu na maafisa kadha wa serikali.

  • Tags

You can share this post!

Wabunge wataka kuzima ukiritimba wa Kenya Power

Maoni mseto kuhusu sare mpya za polisi baadhi wakitaka...

T L