• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 11:54 PM
Wafanyabiashara wavuna Maulidi ikikamilika

Wafanyabiashara wavuna Maulidi ikikamilika

Na KALUME KAZUNGU

HAFLA ya mwaka huu ya Maulid iliyoandaliwa katika kisiwa cha Lamu ilinogesha vilivyo biashara na kuwaacha wengi wakiwa na pesa mfukoni.

Hafla hiyo huandaliwa kila mwaka na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu ili kukumbuka kuzaliwa kwa Mtume Mohamed (S.A.W) katika mji mtakatifu wa Mecca mwaka wa 570AD.

Sherehe hizo huadhimishwa kila mwezi wa tatu wa mwaka katika kalenda ya Kiislamu.

Hafla ya mwaka huu ambayo ni ya awamu ya 134 tangu kuzinduliwa kwake kisiwani Lamu, ilihudhuriwa na zaidi ya wageni na watalii 7000 kuanzia Jumanne na kukamilika Ijumaa.

Wafanyabiashara wa sekta ya usafiri wa baharini, angani na barabarani, wamiliki wa hoteli, wachuuzi, wakiwemo wale wa mishkaki waliozungumza na Taifa Leo Ijumaa walikiri kuvuna pakubwa katika kipindi chote cha sherehe za Maulidi Lamu.

Ahmed Bakari ambaye ni nahodha wa boti kisiwani Lamu, alisema wiki ya Maulidi ilifufua pakubwa biashara, hasa ya boti na mashua kwani wageni waliohudhuria Maulidi walikodi boti na mashua zao kusafiri kutoka na kuingia kisiwani Lamu.

“Tunashukuru kwani tumevuna faida kubwa. Wateja waliosafiri kwa boti kuja Lamu kuhudhuria Maulid walikuwa wengi. Fedha tulizopata wakati wa Maulidi ni sawa na kufanya kazi karibu mwezi mzima,” akasema Bw Bakari.

Mmiliki wa hoteli ya Bush Gardens, Ghalib Alwy, ambaye pia ni mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Lamu (LTA) alipongeza hafla ya mwaka huu ya Maulidi kwa jinsi ilivyopiga jeki biashara ya hoteli.

Waliohudhuria Maulid ya mwaka huu Lamu pia walipata fursa ya kunufaika kwa kambi ya matibabu ya bure iliyofanyika katika hospitali kuu ya King Fahad mjini Lamu.

You can share this post!

Kamishna aamuru ukaguzi kuzuia bidhaa za magendo kutoka...

Bioteknolojia ina nafasi kubwa katika kukabiliana na...

T L