• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 6:07 PM
Kamishna aamuru ukaguzi kuzuia bidhaa za magendo kutoka Tanzania

Kamishna aamuru ukaguzi kuzuia bidhaa za magendo kutoka Tanzania

Na KNA

KAMISHNA Mshirikishi wa eneo la Pwani , Bw John Elungata, ameamuru vikosi vyote vya usalama eneo hilo kuanzisha operesheni dhidi ya ulanguzi wa bidhaa za magendo kutoka Tanzania.

Alishauri maafisa wa usalama na Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru Nchini (KRA), katika mpaka wa Kenya na Tanzania katika Kaunti ya Kwale, kukagua bidhaa kwa makini.

Bw Elungata aliwataka maafisa wa idara ya forodha katika maeneo ya mpakani ya Vanga na Shimoni kuzuia wafanyabiashara walaghai kuingiza bidhaa nchini bila kulipia ushuru.

“Ukaguzi wa kina wa bidhaa zinazoingizwa nchini kupitia eneo la mpakani kutaimarisha ukusanyaji wa mapato kwa manufaa ya uchumi wa nchi,” Bw Elungata akasema baada ya kutembelea kituo cha mpakani cha Lunga Lunga.

Afisa huyo pia aliongoza mkutano wa usalama katika kituo hicho ambapo suala la bidhaa za magendo lilijadiliwa kwa kina.

“Tunahitaji kuweka mikakati thabiti ya kudhibiti uovu huu wa uingizwaji wa bidhaa nchini na walaghai ambao hukwepa kulipa ushuru,” Bw Elungata akasema.

You can share this post!

Kaunti za Mulembe zilitumia mabilioni kwa ziara –...

Wafanyabiashara wavuna Maulidi ikikamilika

T L