• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 11:39 AM
Wahudumu wa mochari wafutwa kazi

Wahudumu wa mochari wafutwa kazi

NA RUTH MBULA

GAVANA wa Kisii Simba Arati amewafuta kazi wahudumu wawili wa mochari kuhusu madai ya hujuma katika mochari ya Hospitali ya Rufaa mjini Kisii.  

Kiongozi huyo aliyeonekana mwenye hasira aliagiza kwamba wahudumu hao wawili wasindikizwe nje ya mochari hiyo na maafisa wa usalama waliojihami ili wasirejee kituoni humo na kuendelea na vitendo walivyotuhumiwa.

“Watu hawa walikuwa wanasimamia kituo hiki. Walizima mtambo wa barafu na kusababisha miili kuoza. Walifanya hivyo kwa ushirikiano na mahasimu wengine waliokuwa wanapambana kunipiga vita kisiasa,” alisema Gavana Arati.

Gavana wa Kisii Bw Simba Arati, afuta kazi wahudumu wawili wa mochari kufuatia madai ya hujuma katika mochari ya Hospitali ya Rufaa mjini Kisii. PICHA / MAKTABA

Madaktari walisema hawajabaini ni kwa nini miili iliyohifadhiwa katika mochari hiyo ilikuwa inaoza wiki iliyopita, kiasi cha kupata wadudu ilhali kulikuwa na mbinu kadhaa za kuihifadhi.

Iwapo mitambo ya barafu ilikumbwa na hitilafu, wahudumu hao wangetumia kemikali kama vile formalin zinazopatikana hospitalini humo.

“Hata wafu wanastahili heshima. Hatuwezi kuwa tunapiga siasa na wafu. Sote tutakufa siku moja lakini hata tutakapoaga dunia, tutahitaji kupatiwa heshima,” alisema.

Alisema kuwa usimamizi wake umeanzisha uchunguzi katika muda wa wiki moja iliyopita kuhusu madai kwamba mochari hiyo inayochukuliwa kuwa moja kati ya vituo bora zaidi vya umma eneo la Nyanza imesambaratika na kwamba miili iliyopelekwa hapo kuhifadhiwa imeoza vibaya.

  • Tags

You can share this post!

Kinaya wakazi majirani wa bomba kuu kukosa maji safi

Kenya kuandaa Cecafa ya wasiozidi umri wa miaka18

T L