• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 6:50 AM
Kenya kuandaa Cecafa ya wasiozidi umri wa miaka18

Kenya kuandaa Cecafa ya wasiozidi umri wa miaka18

NA AREGE RUTH

KENYA itakuwa mwenyeji wa mashindano ya wanawake ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 18 kuanzia Juni 3-17, 2023.

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) lilisimamisha Kenya mnamo Februari 2022 kutokana na kuingiliwa na serikali.

Marufuku hayo yaliondolewa Novemba 2022.

Kenya ilirejea katika soka ya kimataifa Marchi 28, 2023 wakati Harambee Stars ilipocheza na Iran katika mechi ya kirafiki. Iran ilishinda 2-1 mjini Tehran.

Wakati uo huo, timu ya wanawake Harambee Starlets pia iliingia kambini kujiandaa kwa mechi ya kupimana nguvu na Albania.

Mechi hiyo ambayo ilikuwa imepangwa kusakatwa Aprili 11 jijini Tirana, haikuchezwa kutokana na changamoto za usafiri.

Kulingana na tovuti ya CECAFA, Katibu Mtendaji wake Auka Gecheo alithibitisha kuwa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) litaandaa mashindano hayo

“Tuna Vyama viwili vya Wanachama ambavyo vimetuma maombi ya kuandaa mashindano manne mnamo 2023 na tutawasiliana na waandaji wa mashindano mengine matatu baadaye,” akaongeza Auka Gecheo.

Kenya ambao mara ya mwisho walikuwa wenyeji wa michuano ya CECAFA mwaka wa 2021, pia wametuma maombi ya kuandaa mashindano ya CECAFA ya wanaume ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 18 ambayo yatafanyika mwezi Novemba 25 hadi Desemba 9.

Kando na hayo, CECAFA imeweka wazi kuwa, wenyeji wa mashindano ya shule za Pan Afrika, Kombe la Kagame na michunao ya CECAFA ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23 watatangazwa baadaye.

Shirikisho la Vyama vya Soka Uganda (FUFA), limethibitisha kuwa mwenyeji wa michuano ya CECAFA kwa Vijana wasiozidi umri wa miaka 15 na mechi ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa ya Wanawake (CAF) ukanda huu wa CECAFA.

  • Tags

You can share this post!

Wahudumu wa mochari wafutwa kazi

Kocha Mulee asema Gaspo Women wameweka macho kwa Kombe la...

T L