• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Wanawake wadai kukosa maji ya kuoga kunafanya waume kuwaogopa

Wanawake wadai kukosa maji ya kuoga kunafanya waume kuwaogopa

NA MWANGI MUIRURI

MBUNGE wa Maragua Bi Mary wa Maua ameongoza baadhi ya wanawake wa eneo hilo kujadili suala muhimu la namna ya kudumisha usafi ambapo wamelalamika kwamba kuna tatizo kubwa la maji.

Wanawake hao wamesema kwamba wanalazimika kuwajibika mchana kutwa wakitafuta riziki na kufanya kazi za nyumbani lakini baada ya hapo wanakosa maji ya kuoga kabla ya kuenda kulala.

Katika hali hiyo, mmoja wao amesema waume wao wanaogopa hata kuwa karibu nao.

Katika mkanda wa video ambao umesambaa sana katika mitandao ya kijamii, wanawake hao wana wasiwasi kwamba ikiwa hawatapata maji ili wadumishe usafi, “basi ndoa nyingi zitavunjika”.

Walisema msimu huu wa baridi kali wanawake wengi wanajipata pabaya.

Bi wa Maua anasema kwamba ufisadi na uongozi mbaya katika baadhi ya kampuni za usambazaji maji mashinani ndio kiini cha mahangaiko hayo.

Ndipo akachukua jukumu la kuwaongoza wanaume na wanawake waliohudhuria kikao hicho kuomba kupitia nyimbo Mungu awape suluhu ya changamoto inayowakabili.

  • Tags

You can share this post!

Koth Biro: Leads United watuma salamu kwa wapinzani wao

Mpasuko watishia kusambaratisha ODM Kakamega

T L