• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 8:55 PM
Koth Biro: Leads United watuma salamu kwa wapinzani wao

Koth Biro: Leads United watuma salamu kwa wapinzani wao

NA JOHN KIMWERE

KOCHA wa Leads United, Winston Issa amesema kuwa wapo tayari kukabili wapinzani wao kwenye mechi za makala ya 46 kuwania taji la Koth Biro ambazo zimeratibiwa kukunjua jamvi wiki ijayo.

Mwenyekiti wa kipute hicho, Paul ‘Polosa’ Ojenge amesema kuwa kwa sababu ya muda ngarambe ya msimu huu itashirikisha timu 32 pekee kinyume na miaka iliyotangulia.

”Raundi hii nimepanga wachezaji wangu vizuri tayari kuonana macho kwa uso na wapinzani wetu, lengo kuu likiwa kubeba taji hilo wala sio kumaliza nafasi ya pili kama msimu uliopita,” kocha wa Leads United amesema na kuongeza kuwa anafahamu bayana kuwa wapinzani wao wamepania kushusha ushindani mkali.

Anasisitiza kuwa ingawa hawajafahamu ni timu gani na gani zitakaoshiriki kipute cha mwaka huu 2023, ana imani kwamba vikosi vingi vimejipanga kuwakabili kwa kuzingatia miaka ya hivi karibuni wao ndiyo wapinzani wakuu.

Kwenye kampeni za muhula uliopita (2022), Leads United walimaliza katika nafasi ya pili walipozabwa mabao 4-2 na Team Korongez kupitia mikwaju ya penalti baada ya kutoka nguvu sawa kwa kufungana 1-1 katika muda wa kawaida kwenye fainali.

Kwenye ngarambe iliyotangulia (2021), kulikosekana mshindi pale wafuasi wa Borussia FC walivuruga kwa kuzua fujo baada ya kikosi hicho kutoka sare tasa na Leads United.

Shindano hilo huvutia wachezaji wa klabu za ligi tofauti hapa nchini.

  • Tags

You can share this post!

Maandamano ya Azimio yalivyosambaa Saba Saba

Wanawake wadai kukosa maji ya kuoga kunafanya waume...

T L