• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 6:39 PM
Watu wanne wafariki kwa kuangukiwa na mbao za ghorofa inayoendelea kujengwa Pangani

Watu wanne wafariki kwa kuangukiwa na mbao za ghorofa inayoendelea kujengwa Pangani

NA WINNIE ONYANDO

WATU wanne wameaga dunia baada ya kuangukiwa na mbao katika ghorofa moja inayojengwa Pangani, Nairobi

Wengine wanane pia walijeruhia katika mkasa huo.

Kulingana na kamanda wa polisi eneo la Starehe Bw William Sirengo, watu wanne walikufa papo hapo na waliojeruhiwa wakapelekwa katika hospitali zilizo karibu.

“Huu ni mkasa wa kushangaza sana. Waathiriwa waliojeruhiwa walikimbizwa katika vituo tofauti vya matibabu, huku waliohitaji matibabu ya dharura wakikimbizwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta. Watatu walipelekwa katika hospitali ya Abyan, wawili hospitali ya hapa karibu, na wengine watatu MSF. SGBV/Kliniki ya Huduma ya Matibabu ya Dharura,” Bw Sirengo ameambia Taifa Jumapili.

Hata hivyo, Mzee wa Kijiji wa Pangani Bw Jeremiah Kioko ametupilia mbali ripoti za polisi akisema kwamba zaidi ya watu 10 walipoteza maisha katika mkasa huo.

“Watu sita walifariki papo hapo, wanne walikimbizwa katika hospitali iliyo karibu na wengine wakakimbizwa Kenyatta. Ninaamini kwamba idadi ya watu waliopoteza maisha ni kubwa zaidi, ikizingatiwa kutokuwepo kwa ukaguzi kutoka kwa Mamlaka ya Kitaifa ya Ujenzi ili kutathmini usalama wa eneo hilo,” Bw Kioko alisisitiza.

Anaiomba serikali kuhakikisha jengo lote linalojengwa katika eneo hilo linakaguliwa.

“Tunaiomba serikali kuchukua hatua dhidi ya mmiliki wa jengo hilo na kuhakikisha kuwa ukaguzi wa kina unafanywa kwenye maeneo yote ya ujenzi,” alisema na kuongeza kuwa baadhi ya majengo katika eneo hilo hujengwa ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.

  • Tags

You can share this post!

Itumbi akanusha madai kwamba Rais Ruto kaandamana na ujumbe...

Serikali kupendekeza sheria ya kudhibiti soko la hewa ukaa...

T L