• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 4:40 PM
AU yataka vijana watumie teknolojia kutatua shida zao

AU yataka vijana watumie teknolojia kutatua shida zao

NA CECIL ODONGO

UMOJA wa Afrika (AU) umesema uvumbuzi wa kiteknolojia ndiyo nguzo kuu ambayo inastahili kukumbatiwa na vijana kusuluhisha matatizo mengi yanayozonga Bara la Afrika.

Mkurugenzi wa Masuala ya Wanawake, Jinsia na Vijana kwenye AU Prudence Ngwenya Ijumaa, Novemba 17, 2023 alisema vijana sasa wanastahili kukumbatia matumizi ya teknolojia ili kusuluhisha matatizo yanayowakabili.

Ni kupitia njia hiyo Afrika itastawi kiuchumi na kupiga hatua kimaendeleo.

Teknolojia: Samuel Muthui, kutoka Meved Dairy Farm Kirinyaga akielezea kuhusu matumizi ya apu ya kidijitali katika kuendeleza ufugaji. PICHA|SAMMY WAWERU

“Mambo sasa yanabadilika kila kukicha na ni uvumbuzi wa kiteknolojia utasaidia kusuluhisha matatizo ibuka. Huu ndio mwelekeo ambao unastahili kukumbatiwa na vijana,” akaongeza Bi Ngwenya.

Afisa huyo wa AU alikuwa akizungumza jana kwenye Hoteli ya Boma alipofungua Kongamano la siku tatu la YMCA ambalo lilishirikisha mataifa 24 ya Afrika.

“Tunaendeleza miradi mbalimbali ili vijana wawe mabalozi bora. Pia tunaendesha mafunzo ya kiufundi ili kupata njia bora ya kuwasaidia vijana wanaopitia changamoto mbalimbali,” akasema Bw Musima.

Teknolojia ya kisasa kuendeleza ufugaji. PICHA|SAMMY WAWERU
  • Tags

You can share this post!

Familia yahangaikia Sh300,000 kurejesha mwili wa jamaa...

Barabara yakatika kufuatia mvua na kuacha wanakijiji 3,000...

T L