• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Diwani maalum apinga kutimuliwa

Diwani maalum apinga kutimuliwa

Na RICHARD MUNGUTI

DIWANI maalum Kaunti ya Nyamira Bi Mitchel Kemuma ameomba Mahakama Kuu itupilie mbali rufaa aliyokata mkazi kutoka Kiambu anayepinga uteuzi wake na Chama cha Jubilee Septemba 9, 2022.

Uteuzi wa diwani huyo unapingwa na Bi Dolphine Nyang’ara Onkoba, ambaye anamezea mate wadhifa huo.

Wakili Ndubi Mokua alimweleza Jaji Mwihaki Njuguna kwamba uteuzi wa Bi Kemuma kuambatana na agizo la jopo la kuamua mizozo ya vyama vya kisiasa (PPDT) kwamba Jubilee (JPK) ibadilishe orodha ya majina iliyowasilisha kwa tume ya uchaguzi IEBC kuteuliwa kuwa madiwani maalum.

Jaji Mwihaki alifahamisha katibu mkuu wa JPK aliandikia IEBC akiomba majina yabadilishwe lakini haikutekeleza agizo la PPDT.

Bw Mokua alisema kufuatia uamuzi wa PDT Bi Kemuma aliteuliwa.

Pia wakili huyo alitetea uamuzi wa mahakama ya Nyamira ukiratibisha uteuzi wa Bi Kemuma.

Lakini wakili Wilkins Ochoki alisema hakimu mkazi William Chepseba alikosea kuratinisha uteuzi wa Bi Kemuma.

Bw Ochoki alisema kubadilishwa kwa orodha ya uteuzi wa madiwani maalum na JPK ulikinzana na sheria za uchaguzi.

“Naomba hii mahakama ibatilishe uteuzi wa Bi Kemuma na kumtangaza Dolphine Nyang’ara Onkoba diwani maalum kaunti ya Nyamira,” Bw Ochoki aliomba korti.

Alisema kulikuwa na orodha mbili za majina ya uteuzi.

Lakini Bw Mokua alitetea uamuzi wa Bw Chepseba akisema ulikuwa halali na kuomba Jaji Njuguna atupilia mbali rufaa ya Bi Onkoba akisema haina mashiko kisheria.

Kesi hiyo itaendelea Mei 16 mahakama ifahamishwe ikiwa IEBC iwasilishe kortini Sh100, 000 kusimamia gharama za kesi hiyo.

  • Tags

You can share this post!

Pasta Ezekiel Odero abadili nia

Makanisa, wafanyikazi wakataa ushuru mpya

T L