• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 2:33 PM
Pasta Ezekiel Odero abadili nia

Pasta Ezekiel Odero abadili nia

Na RICHARD MUNGUTI

HAKIMU mkazi mahakama ya Milimani Ben Mark Ekhubi Ijumaa alisitisha kuamua ikiwa akaunti 28 za Pasta Ezekiel Odero zitafunguliwa, ili kusubiri uamuzi wa Mahakama kuu Mombasa kuhusu suala hilo.

Bw Ekhubi alisitisha kusoma uamuzi wake baada ya mawakili Danstan Omari, Sam Nyaberi na Cliff Ombeta kumsihi asubiri uamuzi utakaosomwa na Jaji Olga Sewe.

“Baada ya kuhoji suala hili la kufunguliwa kwa akaunti tumemshauri Pasta Odero tumefikia uamuzi usitishe kusoma uamuzi wako hadi pale Mahakama kuu ya Mombasa itakaposoma uamuzi wake kuhusu kufunguliwa kwa akaunti za Pasta Odero,” Bw Nyaberi alimweleza Bw Ekhubi.

Hakimu Ben Mark Ekhubi anayesikiza kesi dhidi ya Pasta Ezekiel Makenzie. Picha/ Richard Munguti

Akaunti za Pasta huyo zilifungwa na polisi wanaomchunguza kwa kutekeleza uhalifu wa kutoa mafunzo ya itikadi kali kwa wafuasi wake, mauaji na ulanguzi wa pesa.

Alhamisi Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma alipinga kesi aliyowasilisha Pasta Odero akiomba akaunti zake zifunguliwe akisema wanafunzi zaidi ya 3, 000 wanaodhaminiwa na kanisa lake wanaumia.

Bw Ekhubi alisema mahakama kuu iko na mamlaka juu ya korti za mahakimu na “ni jambo la busara kusubiri maagizo ya mahakama kuu.”

Omari na Ombeta walimshtaki Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Jinai DCI na Inspekta General wa Polisi Japheth Koome kwa kufunga akaunti za Kanisa na za Pasta huyo.

Jaji Olga Sewe wa Mahakama kuu ya Mombasa aliyeamuru wiki iliypopita ibada katika kanisa la Pasta Ezekiel ziendelee ataamua Mei 17, 2023 ikiwa akaunti hizo zitafunguliwa.

Pasta huyo alikamatwa baada ya Muhubiri Paul Mackenzie kutiwa nguvuni na kuzuiliwa polisi wakichunguza mauaji ya watu waliozikwa kwa msitu wa Shakahola wa ekari 850.

  • Tags

You can share this post!

Ulinzi Starlets kuvaana na Kispeed Queens kombe la FKF

Diwani maalum apinga kutimuliwa

T L