• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 7:50 AM
Gachagua awaomba Wakenya kuvumilia ugumu wa maisha serikali ikilainisha mambo

Gachagua awaomba Wakenya kuvumilia ugumu wa maisha serikali ikilainisha mambo

Na STEVE NJUGUNA

NAIBU Rais Rigathi Gachagua amewahimiza Wakenya waendelee kuvumilia wakijaribu kufufua uchumi.

Huku akionekana kuutetea Mswada wa Fedha 2023, Bw Gachagua alisema ni sawa kwa serikali kufanya maamuzi magumu na yasiyopendeza kwa manufaa ya watu wake.

Bw Gachagua alibainisha kuwa pindi tu Bunge la Kitaifa litakapopitisha Mswada huo, utasaidia serikali kupata pesa kufufua uchumi.

“Kwa sasa tuna deni la Sh9.6 trilioni. Kwa hivyo ni lazima tukusanye ushuru wa kujenga barabara na kuendeleza miradi mingine. Pesa hizo hatutazipata kupitia mkopo,” akasema Bw Gachagua akiwa katika Kanisa la Kianglikana la Nyahururu Kaunti ya Laikipia.

“Ili mambo yabadilike lazima watu waumie kidogo. Hii ndiyo maana tunaomba Wakenya watupe muda ili tusuluhishe masuala ya kupanda kwa gharama ya maisha.”

Alisema kuwa utawala wa Kenya Kwanza unawawazia Wakenya mema na kwamba serikali inalenga kuboresha uchumi.

“Hatuna mpango wa kuwaacha Wakenya watumbukie shimoni.”

  • Tags

You can share this post!

Waziri Kindiki: Tutafanya maombi Shakahola kuondoa laana

Wawili wakamatwa wakisafirisha bangi yenye thamani ya...

T L