• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 7:50 AM
Karua apoteza raundi ya 2 katika kesi ya Waiguru

Karua apoteza raundi ya 2 katika kesi ya Waiguru

Na RICHARD MUNGUTI

JARIBIO la kinara wa Chama cha Kisiasa – Narc Kenya Bi Martha Karua kumshtaki Gavana wa Kirinyaga na maafisa wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kwa makosa ya uchaguzi mkuu wa 2017 lilikataliwa na mahakama.

Hakimu mwandamizi wa mahakama ya Milimani Bi Zainab Abdul alikataa ombi la Bi Karua akisema “mlalamishi (Karua) hakupiga ripoti kwa polisi kuhusu madai ya utoaji hongo kwa wapigakura na maajenti wa Bi Waiguru.

”Bi Abdul alisema mlalamishi hakuwasilisha ushahidi mahakamani kuonyesha jinsi Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji na Inspekta Jenerali wa Polisi (IG) na Mwanasheria Mkuu walishindwa kuwakamata na kuwashtaki washukiwa hao.Bi Abdul alisema kuwa mshtakiwa hakuwasilisha ushahidi wowote kuthibitisha DPP, IG na Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Jinai (DCI) George Kinoti walikataa kutekeleza majukumu yao ya kikazi.

Karua alidai utoaji hongo ulifanyika katika vituo vya kupiga kura katika shule ya upili ya Baricho, shule ya msingi za Kang’aru na Sagana miongoni mwa vituo vingine.

You can share this post!

Nchi chache Afrika zatenga fedha za kutosha kwa sekta ya...

Ruto apiga chenga Raila, Uhuru kuhusu mswada

T L