• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:05 PM
Nchi chache Afrika zatenga fedha za kutosha kwa sekta ya afya

Nchi chache Afrika zatenga fedha za kutosha kwa sekta ya afya

Na PAULINE ONGAJI

Nchi wanachama wa Muungano wa Afrika zilipokutana jijjini Abuja, Nigeria, Aprili 2001, zilikubaliana kutenga asilimia 15 ya bajeti ya serikali zao kwa afya.

Ahadi hii kwa jina Azimio la Abuja (Abuja Declaration) ilikuwa jukwaa la mataifa ya Afrika kukusanya na kutenga rasilimali zao kutoka ushuru na kutengea sekta ya afya.Hii ilikuwa kwa sababu rasilimali zaidi zilihitajika kuangazia changamoto za kiafya wakati huo kama vile virusi vya HIV na Ukimwi, maradhi ya Malaria na Kifua kikuu.

Lakini japo katika kipindi cha hivi majuzi baadhi ya mataifa ya Afrika yameongeza kiwango cha fedha zilizotengewa afya, ni nchi chache ambazo zimetimiza shabaha katika mwaka wowote ule. Kwa mfano, mwaka wa 2018 ni nchi mbili pekee zilizofikia shabaha hiyo.

Kwa sasa mataifa ya Afrika hutumia kati ya dola 8(Sh800) na dola 129 (Sh12,900) kwa kila mtu kwa afya, ikilinganishwa na mataifa tajiri ambayo hutumia zaidi ya dola 4,000 (Sh400,000). Hii ni kwa kutokana na masuala mbali mbali kama vile kiwango cha chini cha jumla ya pato la taifa (GDP) na kiwango cha chini cha ukusanyaji thabiti wa ushuru.N

a japo katika miaka ya hivi majuzi bara la Afrika limeshuhudia ongezeko la kiwango cha ukuaji wa kiuchumi, hii haijamaanisha kwamba fedha zilizotengewa afya ziliongezeka.Kwa mfano, kati ya mwaka wa 2001 na 2015, fedha zilizotengewa afya katika mataifa 21 barani kilipungua, na wataalamu wanahoji kwamba huenda hali ikazidi kuwa mbaya wakati huu wa mkurupuko wa maradhi ya Covid 19.

You can share this post!

KINYUA BIN KINGORI: Wakenya wasipuuze chanjo ya corona...

Karua apoteza raundi ya 2 katika kesi ya Waiguru

T L