• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:05 PM
Kaunti saba kukosa stima – Kenya Power

Kaunti saba kukosa stima – Kenya Power

NA BENSON MATHEKA

KAMPUNI ya Kenya Power imetangaza hitilafu kubwa itakayoathiri kaunti saba zikiwemo Nairobi, Mombasa, Kiambu, Makueni, Murang’a, Nyeri na Kirinyaga.

Kupotea kwa stima kutaendelea kwa zaidi ya saa kumi, kuanzia saa nane asubuhi hadi saa kumi na moja jioni Jumatano, Agosti 30.

Kampuni ya Kenya Power ilihusisha kupotea kwa stima na kazi iliyoratibiwa ya ukarabati ikibainisha kuwa itafanya kazi kurejesha stima haraka iwezekanavyo.

Hatua hiyo itaathiri idadi ya mitambo jijini Nairobi na maeneo mengine ikiwa ni pamoja na vituo vya polisi, shule na maeneo ya shughuli za kibiashara.

Kaunti ya Nairobi, baadhi ya maeneo yatakayoathiriwa ni Kayole, Saika, Maili Saba, Mwengenye, Obama, Njiru, Slaughter House, Komarock Sector 1, Kayole Junction na Kituo cha Polisi cha Kayole miongoni mwa mengine.

Katika Kaunti ya Mombasa, kukatika kwa stima kutaanza saa tisa asubuhi hadi saa kumi na moja jioni, na kutaathiri Shule ya Msingi ya Mrima, Mount Sinai, Mwananguvuze, Kona Zamani, Harambee, Kona Mpya, Vijiweni, Bububu, Mbuta, Shonda, Ujamaa na Shikaadabu.

Katika Kaunti ya Kiambu, stima ilipotea saa tisa asubuhi hadi saa kumi na moja jioni, na kuathiri sehemu ya Thindigua, Paradise Lost, Runda Palms, Citam, Evergreen.

Katika Kaunti ya Makueni hali huyo itashuhudiwa Soko la Kilala, Soko la Mukuyuni, Ukia, Kivani, Mbuani, Utagwa na Kyamuthei.

Murang’a, maeneo yaliyoathirika ni pamoja na Shule ya Wasichana ya Nginda, Kijiji cha Nginda, Soko la Ihumbu, Shule ya Wasichana ya Kaharo, Shule ya Sekondari ya Gathera, Itaaga, Shule ya Sekondari Itaaga, Soko la Gachocho na Taasisi ya Mafunzo ya Ufundi ya Muranga.

Katika Kaunti ya Nyeri, kukatika kwa stima kumeanza saa nane asubuhi na kunaendelea hadi saa kumi jioni, na kunaathiri Kiawara, Nairutia, Tanyai, Matopeni, Lamuria, Bellevue, Kariguini, Mugunda, Kamiruri, Marina na Mahiga Meru.

  • Tags

You can share this post!

Utata Gabon wanajeshi wakifuta matokeo ya urais

Nyongeza za walimu kuchotwa na makato ya nyumba na NSSF

T L