• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 8:50 AM
Utata Gabon wanajeshi wakifuta matokeo ya urais

Utata Gabon wanajeshi wakifuta matokeo ya urais

BENSON MATHEKA Na MASHIRIKA

LIBREVILLE, GABON

GABON inashuhudia wingu jeusi baada ya dazani ya wanajeshi kujitokeza kwa runinga ya kitaifa na kutangaza kwamba hawakubaliani na matokeo ya kura za urais yaliyoonyesha Rais Ali Bongo Ondimba ndiye mshindi.

Tume ya uchaguzi nchini humo, mnamo Jumatano imemtangaza Rais Bongo mshindi, ikisema alijizolea asilimia 64.27 ya jumla ya kura halali zilizopigwa, akimshinda Albert Ondo Ossa, aliyemfuata akiwa na asilimia 30.77 ya kura.

Akitangaza matokeo hayo, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi – Gabonese Elections Centre – Michael Stephane Bonda, amesema wagombea wengine 12 waligawana asilimia iliyobaki.

Idadi ya waliojitokeza kupiga kura mnamo Jumamosi, Agosti 26, 2023, ilikuwa asilimia 50.65.

Lakini mara baada ya kutangaza matokeo hayo, wanajeshi wamejitokeza kwa kituo cha runinga cha Gabon 24 wakisema wanazungumza kwa niaba ya ‘Kamati ya Mpito na Urejeshaji wa Hadhi ya Asasi’.

“Tumeona tabia isiyokubalika, utawala usiotabirika unaohatarisha mfumbato wa kijamii na unaoweza kusababisha ghasia na machafuko… tumeamua kudumisha amani kwa kutamatisha utawala ulioko madarakani,” amesema mwanajeshi mmoja.

Milio ya risasi imesikika katika jiji kuu la Libreville.

Mwanajeshi mwingine amesema mipaka yote ya nchi hiyo imefungwa kwa sasa.

  • Tags

You can share this post!

Serikali yaondoa hitaji la vitambulisho kwa wanafunzi...

Kaunti saba kukosa stima – Kenya Power

T L