• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 3:55 PM
Mahakimu na majaji hawajapokea nyongeza za mishahara

Mahakimu na majaji hawajapokea nyongeza za mishahara

Na RICHARD MUNGUTI

CHAMA cha majaji na mahakimu (KMJA) jana kilikanusha kwamba wanachama wake wamepokea mamilioni ya pesa kama nyongeza ya mishahara.

Rais wa KMJA Bw Derrick Kuto alisema jana tume ya kushughulikia mishahara ya watumishi wa umma (SRC) haijawaongeza mishahara kama inavyodai. “Tangu 2019 hakuna hata jaji au hakimu mmoja amepata nyongeza ya mshahara,” alisema Bw Kuto katika Mahakama ya Milimani.

Bw Kuto ambaye ni hakimu alifichua kwamba mahakimu hupokea mshahara wa Sh90,000. Alifichua mahakimu hawana ulinzi, hawana marupurupu ya kununua nyumba ama magari. “Mahakimu wanaishi maisha ya uchochole,”alisema Bw Kuto.

Aliomba SRC iwaongezee mishahara waimarishe maisha yaona kufanyakazi pasi bughudha.

You can share this post!

Kongamano lajadili mfumo bora wa afya

Hakuna sherehe za pombe haramu

T L