• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 12:18 PM
Mbunge afichua kanisa Nairobi waumini hushiriki ngono bila kinga baada ya kulishwa chakula cha kiroho

Mbunge afichua kanisa Nairobi waumini hushiriki ngono bila kinga baada ya kulishwa chakula cha kiroho

Na MWANGI MUIRURI

MBUNGE wa Maragua Bi Mary wa Maua Jumapili, Juni 18, 2023 alidai kuwa anajua kanisa moja Jijini Nairobi lenye matawi nchini ambapo kuanzia saa nane mchana huwa ni wakati wa washirika kujamiiana.

“Kuanzia saa nane mchana, washirika huwa wanatoa nguo na kubakia uchi wa mnyama kisha wanashiriki ngono ndani ya kanisa,” akasema katika kanisa la
Pentecostal Evangelistic Fellowship of Africa (PEFA) lililoko katika mtaa wa Kamahuha, Kaunti ya Murang’a.

Mgeni wa heshima katika kanisa hilo alikuwa Waziri wa Usalama wa Ndani Profesa Kithure Kindiki.

Bi Wa Maua alizua msisimko wakati aliambia Prof Kindiki awaze na awazue hali hiyo ingekuwa ndiyo inatekelezwa katika kanisa la PEFA.

“Waziri tafakari hili…Saa nane itupate hapa na tuamrishwe kutoa nguo tubaki uchi. Lile tunda la Adamu na Hawa sasa tuanzane nalo hapa.

“Mimi ikiwa nimekuwa nikikutamani…Na wewe na huyo, yule…Matunda yaliyo hapa sasa yawe ni yetu kumegana,” akasema, akisababisha washirika wa kanisa kuangua kicheko.

Bi wa Maua alimtaja pasta wa kanisa hilo kuwa mfano wa Ibilisi katika himaya ya Jehanamu “na ndiyo sababu tunaunga mkono kikamilifu msako dhidi ya makanisa yanayoshirikisha uhaini wa kidini.”

Bi Wa Maua aliongeza kuwa sheria za kudhiibiti imani hapa nchini ni lazima ziundwe bungeni.

[email protected]

  • Tags

You can share this post!

Wakristo Mwea wadaiwa kukumbatia ushirikina, nyuki...

Kindiki aonya Azimio kuhusu maandamano ya kupinga nyongeza...

T L