• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Mudavadi avuliwa wadhifa wa msemaji wa Waluhya

Mudavadi avuliwa wadhifa wa msemaji wa Waluhya

Na CHARLES WASONGA

KIONGOZI wa ANC Musalia Mudavadi amevuliwa wadhifa wa msemaji wa jamii ya Waluhya na mahala pake kuchukuliwa na Naibu Kiongozi wa ODM Wycliffe Oparanya.

Katika tangazo lililotolewa Ijumaa, Desemba 31, 2022 na Baraza la Wazee wa eneo la Magharibi katika uwanja wa Bukhungu, Kakamega, Gavana huyo wa Kakamega alitwika wajibu wa kuwakilisha masilahi ya jamii hiyo ya Mulembe katika ngazi ya kitaifa.

“Wazee wa eneo la magharibi wanamwasilisha Gavana Wycliffe Ambetsa Oparanya kama kiongozi wa jamii ya Waluhya kwako Raila Odinga, ili awakilishe masilahi ya jamii yetu katika serikali utakayounda mwaka 2022,” ikasema taarifa ya azimio hilo la wazee.

Bw Mudavadi, ambaye alialikwa katika mkutano huo lakini akadinda kuhudhuria, amekuwa akishikilia wadhifa huo wa msemaji wa Waluhya kuanzia mwaka wa 2016.

Alitwikwa taji hilo katika uwanja huo huo wa Bukhungu mnamo Desemba 31, 2016 katika mkutano ambao ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa jamii ya Waluhya.

Mkutano huo, sawa na wa mwaka huu ambao Bw Mudavadi na kiongozi wa Ford Kenya Moses Wetang’ula walikataa kuhudhuria licha ya kualikwa, uliandaliwa na Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi Nchini (COTU) Francis Atwoli.

You can share this post!

Joao Cancelo wa Man-City avamiwa na wahalifu wanne

Viongozi wafokea wabunge kwa kupigana bungeni

T L