• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 5:55 AM
Ndindi Nyoro aongoza orodha ya wabunge wachapakazi  

Ndindi Nyoro aongoza orodha ya wabunge wachapakazi  

NA WANDERI KAMAU

MBUNGE Ndindi Nyoro wa Kiharu, katika Kaunti ya Murang’a, ameorodheshwa kuwa mbunge bora nchini kiutendakazi, kulingana na ripoti iliyotolewa Jumapili, Oktoba 5, 2023 na shirika la utafiti la Infotrak.

Bw Nyoro, anayehudumu kwa muhula wa pili, aliibuka bora kwa kuzoa asilimia 70.

Nyoro alifuatwa kwa ukaribu na mbunge Peter Kihungi (Kangema), ambaye pia anatoka katika kaunti ya Murang’a, aliyezoa alama 68 (asilimia).

Ijapokuwa utafiti huo uliangazia wabunge 50 bora kiutendakazi, wabunge kumi walioibuka bora ni: John Mwirigi (Igembe Kusini-asilimia 66), Gideon Mulyungi (Mwingi-asilimia 66), Christopher Wangaya (Khwisero-asilimia 66), Robert Mbui (Kathiani-asilimia 66), Peter Kaluma (Homa Bay-asilimia 66), Makali Mulu (Kitui ya Kati-asilimia 65), Geoffrey Wandeto (Tetu-asilimia 65) na Githua Wamacukuru (Kabete-asilimia 65).

Utafiti huo pia uliangazia utendakazi wa wabunge kimaeneo.

Katika eneo la Mashariki, wabunge Mwirigi, Mulyungi na Mbui ndio walioorodheshwa bora mtawalia.

Katika eneo la Kati, wabunge Nyoro, Kihungi na Wandeto ndio walioibuka kidedea dhidi ya wenzao.

Eneo la Pwani, mbunge Omar Mwinyi (Changamwe) ndiye aliyeorodheshwa kuwa bora. Alifuatwa na wabunge Danson Mwakuwona (Wundanyi) na Mohamed Ali (Nyali).

Katika eneo la Bonde la Ufa, mbunge Naisula Lesuuda (Samburu Magharibi) ndiye aliyeibuka bora. Alifuatwa na wabunge Victor Kipng’etich (Chepalungu) na Kuria Kimani (Molo) mtawalia.

Katika eneo la Kaskazini Mashariki, mbunge Abdirahman Huseinweytan (Mandera Mashariki) ndiye aliyeibuka bora, huku akifuatwa na wabunge Adow Mohamed (Wajir Kusini) na Abdi Ali (Ijara).

Katika eneo la Magharibi, Bw Wangaya ndiye aliyeibuka mbunge bora. Alifuatwa na wabunge Peter Salasya (Mumias Mashariki) na Oku Kaunya (Teso Kaskazini).

Katika eneo la Nairobi, mbunge Babu Owino (Embakasi Mashariki) ndiye aliyeorodheshwa bora, huku akifuatwa na wabunge Tim Wanyoyi (Westlands) na Benjamin Gathiru (Embakasi ya Kati).

Katika eneo la Nyanza, Bw Kaluma ndiye alitajwa kuwa bora. Wale waliomfuata ni Charles Were (Kasipul Kabondo) na Mark Nyamita (Uriri).

Ripoti hiyo, ambayo ilitolewa na Afisa Mkuu Mtendaji wa shirika hilo, Bi Angela Ambitho, pia iliangazia wabunge vijana bora kiutendakazi nchini.

Wabunge vijana walioibuka bora kiutendakazi ni Bw Nyoro, Bw Mwirigi, Bw Aseka, Bw Salasya, Bi Lesuuda, Bw Kimani, Reuben Kiborek (Mogotio), John Kagucia (Mukurwe-ini), Bw Owino na Gideon Kimaiyo (Keiyo Kusini).

Wabunge kumi walioboresha utendakazi wao zaidi ni: Bw Kihungi, Bw Kimani, Michael Wambugu (Othaya), Bi Millie Odhiambo (Suba Kaskazini), Francis Sigei (Sotik), Clive Ombane (Kitutu Masaba), Bi Lilian Gogo (Rangwe), Rahim Dawood (Imenti Kaskazini), Bw Kimaiyo na Bw Kipng’etich.

Wabunge walioibuka bora katika kila kaunti ni: Wanjiku Muhia (Kipipiri-Nyandarua), Bw Wandeto (Tetu-Nyeri), Bw Nyoro (Kiharu-Murang’a), Joseph Gachoki (Kirinyaga ya Kati), Bw Wamacukuru (Kabete-Kiambu), Bw Owino (Embakasi Mashariki-Nairobi), Bw Ali (Ijara-Garissa), Abirahman Mohamed (Mandera Mashariki).

Wengine ni: Bw Mohamed (Wajir Kusini-Wajir), Bw Aseka (Khwisero-Kakamega), Bw Kaunya (Teso Kaskazini-Busia), Majimbo Kalasinga (Kabuchai-Bungoma), Omboko Milemba (Emuhaya-Vihiga), Bw Kaluma (Homa Bay Mjini-Homa Bay), James Nyikal (Seme-Kisumu), Opiyo Wandayi (Unguja-Kisumu), Jhanda Zaheer (Nyaribari Chache-Kisii).

Waliowafuata ni: Bw Nyamita (Uriri-Migori), Bw Ombane (Kitutu Masaba-Nyamira), Kenneth Choni (Ganze-Kilifi), Ndegwa Chiforomodo (Lungalunga-Kwale), Danson Mwashabaki (Wundanyi-Taita Taveta), Bw Ali (Nyali-Mombasa), Mohamed Obo (Lamu Mashariki-Lamu) na Said Buya (Galole-Tana River)).

Wengine waliobuka bora katika kaunti wanakotoka ni: Abraham Kirwa (Mosop-Nandi), Nelson Koech (Belgut-Kericho), Samuel Sakimba (Kajiado Kusini-Kajiado), Adams Korir (Keiyo Kaskazini-Elgeyo Marakwet), Bw Kiborek (Mogotio-Baringo), Irene Njoki (Bahati-Nakuru), Bi Lesuuda (Samburu Magharibi-Samburu), Robert Purkose (Endebess-Trans Nzoia).

Wabunge wengine bora katika kaunti zao ni: Janet Sitienei (Turbo-Uasin Gishu), Kitilai Ole Ntutu (Narok Kusini-Narok), Stephen Wachira (Laikipia Magharibi-Laikipia), Peter Lochakapong (Sigor-Pokot Magharibi) na John Ariko (Turkana Kusini-Turkana).

Utafiti huo ulifanyika kati ya Julai na Septemba mwaka huu katika maeneobunge yote 290, ambapo watu 58,748 walihojiwa.

  • Tags

You can share this post!

KCSE 2023 yaanza usalama ukiimarishwa vituo vya kufanya...

Tanzia watu 11 wakifa kwenye ajali mbaya ya barabara Nakuru...

T L