• Nairobi
  • Last Updated June 2nd, 2024 2:01 PM
Prof Kindiki: Ratiba yangu ya kazi inapangwa na wateja wangu; wahalifu na wahuni    

Prof Kindiki: Ratiba yangu ya kazi inapangwa na wateja wangu; wahalifu na wahuni   

NA SAMMY WAWERU 

WAZIRI wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki amesema shajara ya kazi yake inapangwa na wahuni na wahalifu, aliosisitiza hawana makao nchini chini ya utawala wa serikali ya Kenya Kwanza. 

Prof Kindiki alisema Jumapili, Julai 16, 2023 kwamba hana ratiba maalum kwani wahalifu ndio huamua atakaoenda na hatua zitakazochukuliwa.

Akiwataja kama ‘wateja’ wake, Waziri alisisitiza kuwa hatalegeza msimamo wake katika vita dhidi ya uhalifu, magaidi na wahuni wanaoyumbisha amani ya taifa.

“Shajara yangu inapangwa na watu wengine, na si watu wazuri. Inapangwa na magaidi wa Al Shabaab, wezi wa mifugo na wahalifu,” Prof Kindiki alisema.

Aidha, aliorodhesha Al Shabaab, wezi wa mifugo Bonde la Ufa, wahubiri matapeli, pombe haramu na dawa za kulevya, na maandamano ya muungano wa Azimio la Umoja kama kero inayomkosesha usingizi.

“Hao watu ndio wananipangia kazi kwa sababu ndio wateja wangu.”

Waziri Kindiki hata hivyo alisema makundi aliyotaja hatayapa nafasi.

Alisikitika kuwa maafa yameshuhudiwa, ikiwemo maafisa wa polisi na wa kijeshi (KDF) kuuawa kupitia magaidi wa Al Shabaab na oparesheni kupambana na wezi wa mifugo.

 

  • Tags

You can share this post!

Bloga wa Azimio alalamika kuachiwa ‘kangumu’ na mkewe...

Maandamano: Ni vitisho kila upande

T L