• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:50 AM
Bloga wa Azimio alalamika kuachiwa ‘kangumu’ na mkewe kama ‘lunch’

Bloga wa Azimio alalamika kuachiwa ‘kangumu’ na mkewe kama ‘lunch’

NA SAMMY WAWERU

MWANABLOGU wa Azimio la Umoja, Wahome Thuku mnamo Jumapili, Julai 16, 2023 aligeuka kuwa gumzo la mitandao kufuatia malalamishi ya mkewe kumuachia kitafunio kama chakula cha mchana.

Akielekeza lalama kwenye ukurasa wake rasmi wa Facebook, Thuku alichapisha picha ya kitafunio maarufu kama ‘kangumu’ kilichowekwa kwenye sahani.

“Fikiria, Mama Wambui mchana ameenda ushirika (akimaanisha ushirika wa kanisa) akaachia mzee hii kama chakula cha mchana,” Thuku aliandika.

Mama Wambui ndiye mke wake.

Kilikuwa kitafunio kimoja cha rangi ya kahawia, ambacho kilisababisha gumzo na ucheshi mitandaoni.

Wafuasi wa mwanablogu huyo wa upinzani ambaye pia ni wakili, hawakusita kutoa maoni kupitia safu ya mchango.

“Sasa utafanya nini? Iko tu sawa…Chota maji utengeneze kahawa mkuu,” Phoebe Mwangi alimshauri.

CK Yuri, alimweleza hata ana bahati kwani siku ya Jumapili watu hulishwa chakula cha kiroho.

“Itabidi ukae ngumu…” Frank Karis Karis alimjibu, naye Gitau Njau akitaka kujua sababu za mke wake kuondoka bila kumpikia chakula cha mchana.

Irene Mwehaki aliandika: “Lazima watu wafunge.”

Baadhi walimtania, wakimwambia hiyo ni dalili ya mambo makubwa yaliyoko njiani.

“Huo ni mtego! Kuna bomu mahali inasubiri kulipuka. Anataka uongee kuhusu chakula cha mchana kisha awake,” Kamau Simon alionya.

Naye Deudata Gathoni Joy alihoji huenda Wakili Thuku hakuacha pesa za chakula. “Hata una bahati umepata kitu cha kula.”

Mwanablogu huyo ni mfuasi wa muungano wa upinzani nchini, Azimio la Umoja, na amekuwa akikosoa utawala wa Rais William Ruto.

Azimio inaongozwa na Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga.

Amekuwa akilinganisha Dkt Ruto na Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, akitetea vikali utendakazi wa Kenyatta.

  • Tags

You can share this post!

Idadi ya waliofariki Murang’a baada ya lori kupoteza...

Prof Kindiki: Ratiba yangu ya kazi inapangwa na wateja...

T L