• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:05 PM
Rais Ruto amtaka Mandago, wenzake wabebe msalaba kuhusu wizi wa fedha za wanafunzi kusomea Finland

Rais Ruto amtaka Mandago, wenzake wabebe msalaba kuhusu wizi wa fedha za wanafunzi kusomea Finland

Na WANGU KANURI

RAIS William Ruto amependekeza kuwa viongozi wa Kaunti ya Uasin Gishu walioiba pesa za kuwafadhili watoto kusomea Finland na Canada kubeba misalaba yao.

Akizungumza alipozuru Eldoret, katika kongamano linaloendelea la Ugatuzi, Rais Ruto alitaka viongozi hao wajipange mapema na kurejesha pesa walizoiba lau sivyo wataingia mashakani.

“Sasa mambo ya uchunguzi inaendelea…Wale wote, kama kuna mtu alikula hiyo pesa ajipange kulipa mapema ama ataingia kwa shida. Hakuna maneno ya kubembelezana, pesa ya ng’ombe ya mtu au ile aliuza shamba lazima arudishiwe,” akasema.

Kisha kuongeza, “Lakini hapo mbele wakati uchunguzi utamalizika, mimi nitaona vile nitasaidia watoto waliohusika na maneno haya sababu ni watoto wetu, hawana hatia na ni vile innocent. Lakini sio kumaanisha kuwa wale waliiba pesa watahepa…hapana, hapana.”

Awali, Idara ya Polisi (NPS) ilitoa idhini ya kukamatwa kwa aliyekuwa gavana wa kaunti hiyo ambaye pia ni Seneta Jackson Mandago na viongozi wengine watatu waliokuwa wakifanya kazi katika kaunti hiyo kwa kukataa wito wa kufika kwenye kituo cha polisi cha Nakuru.

Wanne hao wanashtakiwa kwa kutofika mbele ya hakimu mkuu wa Nakuru ili kujibu mashtaka ya wizi, matumizi mabaya ya ofisi na kushirikiana katika uhalifu.

Wiki jana, usimamizi wa kaunti hiyo ulikuwa na kikao na wazazi na wanafunzi ambao walilipa pesa za kufadhili masomo yao katika vyuo vikuu vya Finland na Canada.

Mwezi jana, gavana Jonathan Bii alisema kuwa kaunti haingeweza kurejesha pesa ambazo wazazi hao walikuwa wamelipa kwani akaunti ilikuwa tu na milioni 18.

  • Tags

You can share this post!

Idadi ya watu walioangamia kwenye mkasa wa moto Hawaii...

Mandago akamatwa kwa kashfa ya Sh1.1 bilioni

T L