• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Rais wa LSK ahimiza waandamanaji wafuate sheria

Rais wa LSK ahimiza waandamanaji wafuate sheria

NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Chama cha Wanasheria Nchini (LSK) Eric Theuri ametoa wito kwa waandamanaji kufanya maandamano ya amani, akifafanua kwamba haki ya kuandamana haimruhusu yeyote kukiuka sheria.

Amesema hayo wakati ambapo muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya umesisitiza kwamba maandamano ya siku tatu kuanzia Jumatano hadi Ijumaa yangalipo.

LSK imesema maandamano yanatekeleza wajibu muhimu katika kukuza demokrasia ya taifa lolote.

“Maandamano hutoa fursa muhimu ya walalamishi kutoa malalamiko yao, kushinikiza mageuzi, na kuchochea uundaji wa sera bora. Maandamano yanalindwa na Kifungu 37 cha Katiba ya Kenya,” amesema Bw Theuri.

Ingawa hivyo, amesema mwandamanaji anaweza kuandamana kwa njia ya amani bila kujihami, kukusanyika, kudhihirisha kero yake na kuwasilisha malalamiko yake kwa maafisa wa umma.

Haki hii, amesema inalindwa na haki za kieneo na kimataifa ambazo Kenya ilitia makubaliano kuzitii na ambazo ni Kifungu cha 11 cha Mkataba wa Afrika kuhusu Haki za Binadamu na Watu almaarufu Banjul Charter na Kifungu 21 cha Mkataba wa Kimataifa kuhusu Haki za Kiraia na Kisiasa.

Aidha anashauri kuwepo na mazungumzo baina ya Kenya Kwanza, muungano wa Azimio La Umoja-One na viongozi wa makundi ya kidini.

“LSK tunaweza tukafanikisha mazungumzo ya aina hiyo kwa kuwapa ushauri muhimu wa kitaalamu,” amesema Bw Theuri.

  • Tags

You can share this post!

Viongozi wa Azimio wawarai polisi wakatae ‘kikosi cha...

Ruto akosolewa kupeana hatimiliki kwa wanahisa Embakasi...

T L