• Nairobi
  • Last Updated April 17th, 2024 5:55 PM
Salah aanza kumezea mate dola za Saudi Arabia

Salah aanza kumezea mate dola za Saudi Arabia

Na CECIL ODONGO

Mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah naye anaonekana ashaanza kumezea mate mabilioni ya Saudi Arabia, wiki moja tu baada ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kuanza rasmi.

Duru zinaarifu kuwa Salah ameipa timu moja ya Saudi Arabia idhini ili ianze mazungumzo na Liverpool ndipo naye ajiunge nao mwishoni mwa msimu huu.

Baadhi ya wachezaji wa Liverpool ambao washaagana na timu hiyo na kuendea mabilioni ya mafuta za Saudia ni Roberto Firmino, Fabinho na Jordan Henderson.

Pia kipa wa Liverpool Allison Becker pia anaandamwa na Al Nassr ambayo anaichezea nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo na mshambuliaji wa zamani wa Liverpool raia wa Senegal Sadio Mane.

Mwaka uliopita Liverpool ilirefusha kandarasi ya Salah, 31, hadi 2025 na ni hivi majuzi tu ambapo wakala wake Ramy Abbas Issa alinukuliwa akisema kuwa hawangeongeza mkataba wa mwanadimba huyo iwapo walikuwa wakifikiria angeagana na klabu kabla ya muda huo.

Salah, raia wa Misri ni kati ya wachezaji ambao wanategemewa sana na kocha Jurgen Klopp ambaye analenga kuhakikisha Liverpool wanang’aa msimu huu baada ya kusuasua msimu uliopita.

  • Tags

You can share this post!

Nyota ya Ezekiel yazimwa

Pasta Ezekiel alivyodai wasanii wa Bongo Flava hawana...

T L