• Nairobi
  • Last Updated February 26th, 2024 10:50 AM
Pasta Ezekiel alivyodai wasanii wa Bongo Flava hawana ‘nyota’ ya ndoa

Pasta Ezekiel alivyodai wasanii wa Bongo Flava hawana ‘nyota’ ya ndoa

NA WINNIE ONYANDO

MHUBIRI Ezekiel Odero, wakati wa mahubiri yake yaliyopeperushwa, aliwahi kudai kuwa baadhi ya wanamuziki wa Bongo Flava huenda wakabaki gumegume wa kupachika wanawake mimba bila kuwaoa.

Mhubiri huyo alisema hayo akimwombea mwanaume ambaye alizungumzia jinsi alivyo na mazoea ya kuachana na wanawake wote anaokutana nao hasa baada ya kuwapachika mimba.

Wakati wa mahubiri yake, Mchungaji Ezekiel alitafakari changamoto zinazowakabili wale waliotelekezwa na waume au wake zao na kuachiwa majukumu ya kuwalea watoto.

Papo hapo akamrejelea msanii maarufu wa Bongo Flava bile kumtaja jina.

“Kuna wasanii maarufu wa Bongo ambao wana mazoea ya kuwapa ujauzito wanawake tofauti. Amezaa watoto kadhaa na wanawake tofauti,” mchungaji Ezekiel alihubiri.

Mchungaji huyo alieleza kuwa safari ya maisha ya msanii huyo imemkuta akiwa amezaa watoto na wanawake tofauti na kisha kuwatelekeza.

“Alichukua mmoja kutoka Kenya na kumpachikika mimba kisha kumtupa. Roho ya kuoa hana. Hana roho ya ndoa,” akasema.

  • Tags

You can share this post!

Salah aanza kumezea mate dola za Saudi Arabia

Gachagua adai walinzi wa viongozi wa Azimio waliondolewa...

T L