• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 3:55 PM
 Seneta ashtakiwa kwa kukwepa kulipa ushuru

 Seneta ashtakiwa kwa kukwepa kulipa ushuru

Na RICHARD MUNGUTI

SENETA wa Nakuru aliyepia kinara wa kampuni kutengeneza pombe ya Keroche (KBL) Tabitha Karanja, iliyoko mjini Naivasha ameshtakiwa upya kukwepa kulipa ushuru wa Sh14.5bilioni.

Bi Karanja ambaye pia ni naibu kiongozi wa wengi katika bunge la Seneti alikana mashtaka 10 aliyosomewa mbele ya hakimu mwandamizi Bi Esther Kimilu.

Katika mashtaka mapya yaliyowasilishwa na wakili wa mamlaka ya ushuru nchini KRA Bi Irene Muthee, jina la mumewe Tabitha, Bw Joseph Karanja Muigai lilitolewa kwa vile anaugua.

Punde tu baada ya kusomewa mashtaka hayo mpya, Tabitha aliomba mahakama apewe muda kushauriana na KRA jinsi ya kusuluhisha kesi hiyo nje ya mahakama.

Mshtakiwa alimweleza hakimu “hakuna ushahidi wowote uliotolewa katika kesi hii. Naomba korti inipe fursa ya kusuluhisha kesi hii nje ya mahakama kwa kuweka utaratibu wa kulipa kodi hii kwa mujibu wa sheria za KRA.”

“Katika cheti kipya cha mashtaka tumelitoa jina la Joseph Karanja Muigai, mumewe Tabitha anayeugua na anaendelea na matibabu,” alisema Bi Muthee.

Bi Karanja alikanusha mashtaka yote 10 na kuomba aachiliwe kwa dhamana kama ya kesi ya 2019 iliyofanyiwa marekebisho.

KRA na Bi Karanja wameagizwa na hakimu wasuluhishe mzozo huo wa kodi katika muda wa siku 45 kufikia suluhu.

Kesi itatajwa Juni 5, 2023.

  • Tags

You can share this post!

Maajabu mwanamuziki akila mlo kwenye sahani moja na mbwa  

Maandamano yaendelee sambamba na mazungumzo – Raila

T L