• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Serikali yadhamiria kuzima matumizi ya makaa, kuni katika maeneo ya mijini ifikapo 2028

Serikali yadhamiria kuzima matumizi ya makaa, kuni katika maeneo ya mijini ifikapo 2028

Na CHARLES WASONGA

SERIKALI imetangaza kuwa itazima kabisa matumizi ya kuni na makaa hasa kwa wakazi wa jijini Nairobi na miji mingine mikuu nchini kufikia mwaka wa 2028.

Aidha, Wizara ya Kawi inasema kuna inalenga kupunguza matumizi ya kawi hiyo chafu katika maeneo ya mashambani ambako asilimia 80 wanaitegemea kupikia.

Hii ni licha ya kwamba bei ya gesi ya kupikia inaongezeka kila uchao kufuatia hatua ya serikali kuongeza ushuru unaotozwa bidhaa hiyo.

Lakini Katibu katika Wizara ya Kawi Gordon Kihalangwa, Jumanne alisema serikali imejitolea kuhimiza matumizi ya kawi safi katika upishi licha ya kupanda bei ya gesi.

“Kama serikali tumejitolea kutekeleza mpango wa kukomesha matumizi ya kawi, kama vile kuni na makaa, kupikia katika maeneo ya mijini kufikia mwaka wa 2028,” Meja mstaafu Kihalangwa akasema.

Katibu huyo alisema haya katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na mkurugenzi wa kawi endelevu katika Wizara ya Kawi Bw Dan Marangu katika hafla ya ufunguzi wa Wiki ya Upishi kwa Kawi Safi.

Shughuli hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Jumba la Mikutano ya Kimataifa ya Jomo Kenyatta (KICC), Nairobi.

Kurejelewa kwa ushuru wa zaida ya thamani (VAT), ya asilimia 16, kwa gesi ya kupikia mnamo Julai mwaka huu umechangia ongezeko la bei ya gesi ya kupikia kwa kiwango cha karibu asilimia 24.

Hatua hiyo imewalazimisha wakazi wengi katika mitaa ya mabanda mijini na maeneo ya mashambani wamelazimika kutumia makaa na kuni kupikia. Hali hii, bila shaka, itasababisha ongezeko la visa vya ukataji miti kwa ajili ya kuni na kuni.

Kulingana takwimu za hivi punde kutoka kwa Shirika la Kitaifa la Takwimu (KNBS) inaonyesha kuwa bei ya gesi ya kupikia imepanda kwa asilimia 24 kati ya Oktoba 2020 na Oktoba 2021. Hii ni kwa sababu ya ongezeko la viwango vya ushuru.

Kwa mfano mtungi wa kilo 13 wa gesi unauzwa kwa Sh2,513 bei ya reja reja, mwezi wa Oktoba kutoka Sh2,019 Oktoba 2020.

Hata hivyo, Wizara ya Fedha imedokeza kuwa inapanga kurejesha mpango wa kutoa afueni ya bei ya gesi ya kupikia katika mwaka ujao wa 2022/2023.

Hii, inasema, inalenga kuhakikisha kuwa bidhaa hii inapatikana kwa bei nafuu na Wakenya masikini.

  • Tags

You can share this post!

Man-United wateua kocha Rangnick kushikilia mikoba yao hadi...

Rais Kenyatta ahutubia taifa kupitia kikao cha pamoja...

T L