• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 1:46 PM
Serikali za kaunti kupokea Sh385 bilioni baada ya Rais kutia saini Mswada wa ugavi wa Mapato, 2023

Serikali za kaunti kupokea Sh385 bilioni baada ya Rais kutia saini Mswada wa ugavi wa Mapato, 2023

NA CHARLES WASONGA

SERIKALI za Kaunti sasa zitapokea mgao wa Sh385.4 bilioni katika mwaka ujao wa kifedha wa 2023/2024 baada ya Rais William Ruto kutia saini Mswada wa Ugavi wa Mapato wa 2023.

Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula mnamo Alhamisi, Aprili 27, 2023, aliongoza maafisa wa bunge kushuhudia hafla fupi ya kutiwa saini kwa mswada huo katika Ikulu ya Nairobi.

Kufuatia kutiwa saini kwa mswada huo mgao wa fedha kwa kaunti sasa utaongezeka kwa Sh15.4 bilioni ikilinganishwa na mgao wa Sh370 bilioni ambao ni mgao wa mwaka huu wa kifedha wa 2022/2023.

Mswada wa Ugavi wa Mapato, 2023 unatoa maelezo kuhusu namna mapato yaliyokusanywa kitaifa yatagwanywa kati ya Serikali ya Kitaifa na Serikali za Kaunti kwa mujibu wa mahitaji ya vipengele vya 203 (2) na 218 vya Katiba ya sasa.

Rais Ruto ameutia saini mswada huo siku chache baada ya kupitishwa katika Seneti baada ya mjadala ulioleta mgawanyiko katika ya Maseneta wa Kenya Kwanza na wenzao wa Azimio la Umoja-One Kenya.

Maseneta wa Azimio walitaka serikali za kaunti zitengewe Sh407 bilioni ilhali wale wa Kenya Kwanza watasisitiza kuwa mgao wa Sh385 bilioni unafaa, “kwa sababu uchumi wa Kenya unakabiliwa na changamoto nyingi.”

  • Tags

You can share this post!

Mmea wenye madini mengi kuliko vyakula vyote duniani

Kenya yaweka hai matumaini ya kushinda raga ya Barthes...

T L