• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 6:07 PM
Kenya yaweka hai matumaini ya kushinda raga ya Barthes Trophy kwa kuzima miamba Namibia

Kenya yaweka hai matumaini ya kushinda raga ya Barthes Trophy kwa kuzima miamba Namibia

NA GEOFFREY ANENE

CHIPU ya Kenya ina matumaini ya kunyakua taji la Kombe la Afrika la raga ya wachezaji 15 kila upande (U20 Barthes Trophy) baada ya kunyamazisha Namibia 24-13 katika nusu-fainali kuu ugani Nyayo mnamo Jumatano.

Kocha Curtis Olago na nahodha Laban Kipsang walifurahia ushindi huo ambao ni kisasi kitamu kwa sababu Chipu ilipoteza dhidi ya Wanamibia 16-5 katika nusu-fainali mwaka 2022.

Jackton Omondi alifungia Kenya mguso wa mwisho ulioandamana na mkwaju kutoka kwa Patrick Wainaina.

Nusu-fainali ya pili ni kati ya Kenya na Namibia ilishuhudiwa na mashabiki kiasi cha haja akiwemo Waziri wa Michezo Ababu Namwamba.

Katika nusu-fainali ya kwanza kuu, Zimbabwe ilituma onyo kali kwa wapinzani ilipokung’uta Tunisia 60-6. Tunisia ilikuwa imejibu kila shambulizi katika dakika 10 za kwanza, lakini haikuwa na lake Zimbabwe ilipoanza kuona lango.

Katika mechi za nusu-fainali ya kuorodheshwa nambari tano hadi nane, Cote d’Ivoire iliduwaza Madagascar 16-11 nayo Zambia ikazidia Uganda maarifa 21-13.

Cote d’Ivoire na Zambia zimelimana kuamua nambari tano na sita nazo nafasi mbili za mwisho zitaamuliwa na mechi kati ya Uganda na Madagascar.

Mashindano haya ya mataifa manane yatakamilika Aprili 30, huku mabingwa wakijikatia tiketi ya kushiriki Raga za Dunia za daraja ya pili (World Rugby U20 Trophy) mjini Nairobi mwezi Julai.

Kenya tayari imefuzu kushiriki mashindano hayo ya dunia ya daraja ya pili kwa kuwa ni mwenyeji.

Rais mpya ya Shirikisho la Raga Afrika Herbert Mensah kutoka Ghana anatarajiwa kuhudhuria siku ya mwisho ya mashindano haya ya kila mwaka.

  • Tags

You can share this post!

Serikali za kaunti kupokea Sh385 bilioni baada ya Rais...

Nafasi ya kilimo cha miti kugeuza Kenya kuwa Sweden

T L