• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:50 AM
Taswira ya Tamasha za Kitaifa za Muziki 2023 zinazofanyika Nyeri

Taswira ya Tamasha za Kitaifa za Muziki 2023 zinazofanyika Nyeri

NA SAMMY WAWERU

TAMASHA za Kitaifa za Muziki 2023 zinaendelea kufanyika katika Chuo Kikuu cha Dedan Kimathi, Kaunti ya Nyeri.

Hafla hiyo ilianza mnamo Ijumaa, Agosti 11, 2023 na itaendelea hadi Jumanne, Agosti 22.

Mashindano hayo ya muziki ambayo ni Makala ya 95, yamehudhuriwa na shule mbalimbali nchini, taasisi za elimu ya juu na pia Shirika la Huduma ya Vijana kwa Taifa (NYS).

Nyimbo tofauti za kitamaduni kutoka matabaka mbalimbali nchini, zimetumbuizwa baadhi ya shule na taasisi zikiibuka kidedea katika madaraja ya maigizo.

Vilevile, mashairi yalikaririwa.

Kilele cha mashindano hayo, kitakuwa kutuza washindi katika Ikulu ya Rais, Nakuru.

Aidha, wanatarajiwa kutumbuiza Rais William Ruto ambaye atapokeza makundi bora zawadi na vikombe vya shime.

Mpiga picha wetu Joseph Kanyi, amekuwa akifuatilia tamasha hizo kwa karibu na amenasa mkusanyiko wa picha kueleza taswira ilivyokuwa.

Wanafunzi wa Shule ya Upili ya Wasichana ya Kichaka Simba, kutoka Pwani, wakiwasilisha shairi lenye maudhui ‘Uraia mwema’ wakati wa tamasha za Kitaifa za Muziki katika Chuo Kikuu cha Dedan Kimathi, Makala ya 95. PICHA|JOSEPH KANYI
Wanafunzi wa Shule ya Upili ya Wasichana ya Nginda wakifurahia ushindi wao katika ‘kifungu cha Daraja la 1034J’, wakati wa tamasha za Kitaifa za Muziki katika Chuo Kikuu cha Dedan Kimathi, Makala ya 95. PICHA|JOSEPH KANYI
Wanafunzi wa Shule ya Upili ya Birithia, kutoka Nyeri, wakiwasilisha densi ya Kiskoti (Daraja la 851J) wakati wa tamasha za Kitaifa za Muziki katika Chuo Kikuu cha Dedan Kimathi, Makala ya 95. PICHA|JOSEPH KANYI
Wanafunzi wa Shule ya Upili ya Maria Soti, kutoka eneo la Bonde la Ufa, wakijipiga ‘selfie’ wakati wa tamasha za Kitaifa za Muziki katika Chuo Kikuu cha Dedan Kimathi, Makala ya 95. PICHA|JOSEPH KANYI
Wanafunzi wa Tetu Technical and Vocational College, kutoka Kaunti ya Nyeri, wakiwasilisha densi ya Kikisii wakati wa tamasha za Kitaifa za Muziki katika Chuo Kikuu cha Dedan Kimathi, Makala ya 95. PICHA|JOSEPH KANYI
Wanafunzi wa Eldoret National Polytechnic wakiwasilisha densi ya Kikamba wakati wa tamasha za Kitaifa za Muziki katika Chuo Kikuu cha Dedan Kimathi, Makala ya 95. PICHA|JOSEPH KANYI
Wasomi wa Thika Technical Training Institute, ukumbini na densi ya Kigusii wakati wa Tamasha za Kitaifa za Muziki katika Chuo Kikuu cha Dedan Kimathi, Makala ya 95. PICHA|JOSEPH KANYI
Mcheza pembe hodari wa Shule ya Msingi ya Luoro, kutoka Kaunti ya Migori, akijiandaa kushiriki Tamasha za Kitaifa za Muziki katika Chuo Kikuu cha Dedan Kimathi, Makala ya 95. PICHA|JOSEPH KANYI
Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kasimbiji, kutoka Pwani, wajitosa ukumbini na densi ya Kimijikenda wakati wa Tamasha za Kitaifa za Muziki, Makala ya 95, katika Chuo Kikuu cha Dedan Kimathi. PICHA|JOSEPH KANYI
Wanafunzi wa Taasi ya Tetu Training and Vocational College, kutoka Kaunti ya Nyeri, wakiwasilisha densi ya Kikisii wakati wa Tamasha za Kitaifa za Muziki, makala ya 95, katika Chuo Kikuu cha Dedan Kimathi. PICHA|JOSEPH KANYI
Waamuzi – ‘Majaji’ wakati wa Tamasha za Kitaifa za Muziki, makala ya 95, katika Chuo Kikuu cha Dedan Kimathi. Picha/ JOSEPH KANYI
Wanafunzi wa Sigalagala National Polytechnic wakiwasilisha wimbo ‘Katinde’ ulioimbwa na Jacob Luseno, wakati wa Tamasha za Kitaifa za Muziki, makala ya 95, katika Chuo Kikuu cha Dedan Kimathi. PICHA|JOSEPH KANYI
Vijana wa NYS wakiwasilisha wimbo ‘Muthoni kifagio’ ulioimbwa na Newton Karish, wakati wa Tamasha za Kitaifa za Muziki, makala ya 95, katika Chuo Kikuu cha Dedan Kimathi. PICHA|JOSEPH KANYI
Wanafunzi wa Shule ya Upili ya Wavulana ya Kerugoya wakikariri shairi ‘Club Kenya’ lililoangazia uraia mwema wakati wa Tamasha za Kitaifa za Muziki, makala ya 95, katika Chuo Kikuu cha Dedan Kimathi. PICHA|JOSEPH KANYI
Wanafunzi wa Shule ya Wasichana ya Maria Soti, kutoka Kaunti ya Elgeyo Marakwet, wakiwasilisha shairi ‘Smart Card’ (Daraja la 1035J) wakati wa Tamasha za Kitaifa za Muziki katika Chuo Kikuu cha Dedan Kimathi. PICHA/ JOSEPH KANYI
Wanafunzi wa Shule ya Upili ya Wasichana ya Moi, kutoka eneo la Bonde la Ufa, wakijitosa ukumbini na wimbo wa kitamaduni wa Kimaasai (Daraja la 378) wakati wa Tamasha za Kitaifa za Muziki katika Chuo Kikuu cha Dedan Kimathi. PICHA|JOSEPH KANYI
Wanafunzi wa Shule ya Upili ya Senior Chief Mwangeka, kutoka eneo la Pwani, wakiwasilisha wimbo ‘Akiwom na kitela’ wa Kiturkana (Daraja la 301) wakati wa Tamasha za Kitaifa za Muziki katika Chuo Kikuu cha Dedan Kimathi. PICHA|JOSEPH KANYI
Wanafunzi wa Shule ya Upili ya Wasichana ya State House wakiwasilisha wimbo ‘Najivunia’ (Daraja la 396), wakati wa Tamasha za Kitaifa za Muziki katika Chuo Kikuu cha Dedan Kimathi, Nyeri. PICHA|JOSEPH KANYI
Wanafunzi wa Shule ya Upili ya Wasichana ya Turbo, kutoka eneo la Bonde la Ufa, wakijitayarisha kuwasilisha densi ya Kikeiyo wakati wa Tamasha za Kitaifa za Muziki katika Chuo Kikuu cha Dedan Kimathi, Kaunti ya Nyeri. PICHA|JOSEPH KANYI
Wanafunzi wa Shule ya Upili ya Wasichana ya Tabagon, kutoka Kaunti ya Baringo, wakiwasilisha densi ya jamii ya Kipsigis (Daraja la 373J) wakati wa Tamasha za Kitaifa za Muziki, makala ya 95, katika Chuo Kikuu cha Dedan Kimathi, Nyeri. PICHA|JOSEPH KANYI
Wanafunzi wa Shule ya Upili ya Wasichana ya Iriaini, kutoka Kaunti ya Nyeri, wakisherehekea baada ya shairi lao ‘Ugaidi’ kutajwa kuwa bora zaidi wakati wa Tamasha za Kitaifa za Muziki katika Chuo Kikuu cha Dedan Kimathi, Nyeri. PICHA|JOSEPH KANYI
  • Tags

You can share this post!

Gachagua ashambulia Raila akimtaja kuwa mwelekezi wa...

Mshukiwa wa kutekenya na kupora akijihami kwa shoka atiwa...

T L