• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 7:55 AM
Mshukiwa wa kutekenya na kupora akijihami kwa shoka atiwa mbaroni

Mshukiwa wa kutekenya na kupora akijihami kwa shoka atiwa mbaroni

NA MWANGI MUIRURI

MAAFISA wa polisi katika Kaunti ya Murang’a sasa wanasema wamefanikiwa kumtia mbaroni mshukiwa wa uhalifu, ambaye kwa mwezi mmoja sasa amekuwa akiwapora wenyeji usiku huku akiwa amejihami kwa shoka.

Wengi wa waathiriwa pia wamekuwa wakidai kuwa mshukiwa huyo hupapasa na kubusu anaolenga kupora ili wapitanjia wafikirie yeye na mlengwa ni marafiki.

Wenyeji wamempa mtu huyo jina la majazi la ‘Wagathanwa Muhambati’ yaani, wa shoka mpapasaji.

Kamanda wa polisi wa Murang’a Bw Mathiu Kainga alisema mshukiwa huyo alitiwa mbaroni Ijumaa akiwa katika mahakama ya Kenol alipokuwa ameenda kujibu mashtaka mengine ya uhalifu.

Bw Kainga alisema kwamba “tuko na imani kwamba tumemnasa jambazi sugu na mnamo Jumatatu tutamwasilisha mahakamani kujibu mashtaka ya uvamizi, wizi wa kimabavu na kutishia maisha”.

Aidha, Bw Kainga alisema kuwa mshukiwa huyo anekuwa akivamia boma za watu na kuanzia na kuvunja dirisha kisha anamwaga petroli kwa nyumba.

“Akishamwaga petroli hiyo, anakwambia upitishie yeye pesa na simu kwa dirisha la sivyo arushe moto ndani ya hiyo nyumba,” akasema.

Miongoni mwa waathiriwa wa ujambazi huo ni wakili Mwangi Kamau.

Naye Bi Sarah Wangui, 48, ambaye ni mchuuzi katika soko la Mbombo, anadai kuwa alikutana na mshukiwa mnamo Agosti 12 katika barabara ya kutoka Mbombo kwenda Kamuiru mwendo wa saa tano usiku.

Naye Joseph Kyende ambaye ni kibarua kwa shamba moja eneo la Maragua Ridge, alisema alikumbatiwa, akapigwa busu na kisha kuporwa na mshukiwa huyo mnamo Agosti 13, 2023.

[email protected]

  • Tags

You can share this post!

Taswira ya Tamasha za Kitaifa za Muziki 2023 zinazofanyika...

Kuwa na kambi ya kijeshi Manda hakumaanishi mnatutawala,...

T L