• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 1:13 PM
Tineja mshukiwa wa mauaji ya Eric Maigo kuzuiliwa kwa siku 21

Tineja mshukiwa wa mauaji ya Eric Maigo kuzuiliwa kwa siku 21

NA RICHARD MUNGUTI

MSHUKIWA mkuu katika mauaji ya kinyama ya aliyekuwa kaimu mkurugenzi wa fedha Nairobi Hospital Eric Maigo amefikishwa kortini.

Msichana huyo tineja alifikishwa mbele ya hakimu mwandamizi katika Mahakama ya Milimani Zainab Abdul aliyeamuru azuiliwe kwa siku 21 kuhojiwa na kuchunguzwa.

Maigo alikufa baada ya kudungwa kisu mara 25 kifuani.

Tineja aliyekamatwa Septemba 26, 2023, katika mtaa wa Olympic Kibera, aliagizwa azuiliwe katika kituo cha polisi cha Kileleshwa ambapo Koplo Patrick Boge atamhoji.

Koplo Boge alieleza mahakama kwamba uchunguzi katika kesi hiyo ya mauaji ya Maigo aliyekuwa na umri wa miaka 37 haujakamilika.

Wakili Samuel Ayiro anayemtetea tineja hakupinga ombi la mshukiwa huyo kuzuiliwa kwa siku 21.

“Sipingi ombi la Polisi la kumzuilia mteja wangu kwa siku 21. Uchunguzi kamili ni sharti ufanyike kabla ya mshukiwa kufunguliwa mashtaka ya mauaji,” alisema Ayiro.

Wakili Edward Omotii anayewakilisha familia ya marehemu alisema familia ya mhanga imeumia sana ikitiliwa maanani vyombo vya habari vimeagazia kisa hicho kwa mapana na marefu.

Omotii alieleza korti uchunguzi wa kina ni sharti ufanyike ili haki itendeke.

Akitoa uamuzi, Bi Abdul amesema “polisi wanahitaji kupewa muda wa kuchunguza kwa undani kisa hiki cha mauaji ya kinyama.”

Hakimu pia aliamuru mshukiwa huyo apelekwe hospitalini baada ya wakili Ayiro kusema hajihisi vyema.

Hakimu aliagiza kesi hiyo itajwe kwa maagizo zaidi Oktoba 18, 2023.

Mshukiwa mwingine aliyekamatwa kuhusiana na mauaji hayo ya Maigo ni Cynthia Lusenga Andayo almaarufu Flora Akoth Okonda aliyeachiliwa huru Jumatatu wiki hii baada ya polisi kusema hakuna ushahidi wa kumhusisha na mauaji hayo.

  • Tags

You can share this post!

Nyanya, 71, akiri kuuza mihadarati Kasarani

El Nino: Hofu ya wakazi wa Mukuru-Kayaba jijini Nairobi

T L