• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Uchaguzi nchini Kenya ulikuwa wa kuaminika – Meg Whitman

Uchaguzi nchini Kenya ulikuwa wa kuaminika – Meg Whitman

NA WINNIE ONYANDO

BALOZI wa Amerika nchini Kenya, Meg Whitman, ameshikilia kuwa Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9, 2022, ulikuwa wa kuaminika na kuwa ulikuwa wa uwazi.

“Uchaguzi wa Kenya 2022 ulikuwa wa kuaminika zaidi katika historia,” akasema Balozi Whitman akihutubu kwenye Kongamano la Ugatuzi mjini Eldoret mnamo Jumatano.

Kadhalika, alisisitiza kuwa waangalizi wa ndani na wa kimataifa ambao waliteuliwa kusimamia uchaguzi huo walitekeleza majukulu yao kikamilifu.

“Nilifika Kenya siku chache kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Agosti 2022; uchaguzi huo ulikuwa huru, wa haki na wa kuaminika,” akaongeza Bi Whitman.

Madai hayo yanakuja huku mazungumzo ya maridhiano kati ya mrengo wa Kenya Kwanza na Azimio yakiendelea.

  • Tags

You can share this post!

Kenya Shujaa yaanza maandalizi ya kushiriki Kombe la Afrika

Kutana na mbwa anayepeleka ujumbe wa amani kwa mataifa...

T L