• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 5:26 PM
Kenya Shujaa yaanza maandalizi ya kushiriki Kombe la Afrika

Kenya Shujaa yaanza maandalizi ya kushiriki Kombe la Afrika

Na GEOFFREY ANENE

SHIRIKISHO la Raga Kenya (KRU) limetaja kikosi cha Kenya Shujaa chenye wachezaji 36 kuanza maandalizi ya Kombe la Afrika litakalofanyika jijini Harare, Zimbabwe mnamo Septemba 16-17.

Baadhi ya wachezaji waliong’ara katika duru nne za kwanza za raga za kitaifa za Dala, Driftwood, Prinsloo na Christie wakiwemo Festus Shiasi, Lameck Ambetsa na Fidens Tony wamepata nafasi katika kikosi hicho cha kocha Kevin Wambua.

Mzawa wa Fiji, Jone Kubu, ambaye atakosa duru mbili za mwisho za kitaifa Tisap na Kabeberi akitumikia marufuku ya mechi 11 kwa kukanyaga mpinzani kwenye Christie Sevens wikendi iliyopita, pia amejumuishwa.

Kenya italimana na Zambia, Namibia na Nigeria katika Kundi B kwenye dimba hilo pia la kufuzu kushiriki Olimpiki 2024.

Kundi A linajumuisha Afrika Kusini, Madagascar, Tunisia na Ivory Coast nao mabingwa wa Afrika 2022 Uganda wako Kundi C pamoja na Zimbabwe, Burkina Faso na Algeria.

Kikosi cha Kenya Shujaa: Brian Tanga, Kevin Wekesa, William Mwanjii, Jone Kubu, Lamech Ambesta (Kabras Sugar), George Ooro, Barnabas Owuor, Brunson Madigu, Nigel Amaitsa, Victor Odhiambo (Strathmore Leos), Austin Sikutwa, Vincent Onyala, Elvis Olukusi, Samuel Asati, Festus Shiasi (KCB), Samuel Ovwamu, Floyd Wabwire, Patrick Odongo (Daystar Falcons), Brian Mutugi, Stephen Sikuta, Ronnie Omondi, Tony Omondi, Daniel Taabu, Billy Odhiambo (Mwamba), John Okoth, Beldad Ogeta, Steve Arunga, Dennis Abukuse (Menengai Oilers), Felix Makokha, Herman Humwa, Amon Wamalwa, Paul Mutsami, David Mwangi (Kenya Harlequin), Chrisant Ojwang (Nakuru), Fidens Tony (Nondescripts), Brian Mutua (Homeboyz)

  • Tags

You can share this post!

Raila alivyochezwa

Uchaguzi nchini Kenya ulikuwa wa kuaminika – Meg...

T L