• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Ulevi shule za sekondari wasikitisha

Ulevi shule za sekondari wasikitisha

Na RICHARD MUNGUTI

AFISA mkuu wa Benki ya Equity Dkt James Mwangi ameeleza masikitiko makubwa kuhusu ongezeko la idadi la wanafunzi wa shule za upili wanaotumia madawa ya kulevya.

Dkt Mwangi alighairi kwamba dawa za kulevya zinawaharibu wanafunzi wengi.

Kinara huyo wa Benki ya Equity alitoa wito hatua za haraka zichukuliwe kutatua suala hili.

Akiwahutubia baadhi ya wanafunzi waliofadhiliwa na benki hiyo wakati wa mkutano wa 13 uliofanyika katika shule ya Upili ya Wasichana ya Kangaru, Kaunti ya Embu, Dkt Mwangi alisema dawa za kulevya ni kizingiti kikubwa katika ustawi wa elimu nchini

“Huenda wanafunzi wanawaiga jamaa zao ambao ni waraibu wa dawa za kulevya na walevi wa kupindukia. Watu wazima wanatakiwa kuwa kielelezo chema kwa watoto,” alisema Dkt Mwangi.

Mwanabenki huyu aliwahakikishia wanafunzi zaidi ya 1, 000 wanaofadhiliwa kusoma na benki ya Equity kutoka eneo la Mashariki kwamba wataendelea kupokea ruzuku zao hadi wakamilishe masomo yao.

“Mliofanikiwa kupata msaada huu wa elimu mnatakiwa kusoma kwa bidii na kupata alama za juu katika mitihani kwa vile mahitaji yenu yote yamegharamiwa na benki ya Equity,” alisema Dkt Mwangi.

Pia aliwataka wanafunzi hao wadumishe nidhamu ya hali ya juu ndipo washamiri katika elimu.

  • Tags

You can share this post!

Mbunge wa Gatundu Kusini Kagombe apendekeza hoja ya...

Katibu taabani kwa kula njama za kulaghai

T L